Wahasibu nchini watapatiwa mafunzo ya namna ya kutambua na kuzuia
fedha haramu maarufu kama fedha bandia ili kudhibiti tatizo hilo
ambalo limekuwa likisababisha hasara kubwa katika sekta mbali mbali
nchini.
Mafunzo hayo yatatolewa na kitengo cha udhibiti wa fedha haramu
(financial inteligency ) ambacho kiutawala kiko chini ya wizara ya
fedha ila kikazi wanajitegemea na kufanya kazi na wizara zote.
Akizungumza katika semina ya Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu za
serikali iliyokuwa ikijadili kuhusu soko la mitaji na kutathmini
taarifa za kimahesabu ,maadili ya wahasibu iliyofanyika jijini
hapa.Pius Maneno ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya taifa ya
uhasibu na ukaguzi wa mahesabu (NBA) amesema kuwa semina hiyo
inalenga kutoa mafunzo ya namna ya kutambua fedha haramu na kuzizuia
ikiwa ni mada mojawapo itakayowasilishwa .
“Wahasibu na wakaguzi wa Mahesabu ya serikali watajifunza mbinu mbali
mbali za kutambua fedha haramu na kuzizuia ,mafunzo hayo yatatolewa na
kitengo cha udhibiti wa fedha haramu ambacho kipo chini ya wizara ya
fedha kiutawala ila kiutendaji kinajitegemea na kufanya kazi na wizara
zote kwa kuwa tatizo la fedha haramu haliko katika wizara moja tu liko
katika wizara na sekta mbali mbali” Pius Maneno
Pius Maneno amesema kuwa mbali na hayo semina hiyo itajadili
ushiriki wa soko la hisa ,maboresho ya soko la mitaji na fursa mbali
mbali na pia kutazama changamoto za namna gani Watanzania watawezeshwa
katika soko la mitaji ili liwe kitovu cha uchumi katika maendeleo ya
taifa.
Kwa upande wake Mgeni rasmi aliyefungua semina hiyo Sonford Jacob
Shayo ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya Arusha amesema kuwa
ushirikiano wa Ofisi ya Bodi ya taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa
Mahesabu(NBAA) na Benki kuu ya Tanzania (BOT) unaweza kuleta tija na
kutatua changamoto za zinazowakabili wahasibu na na kuifanya taaluma
hiyo iweze kufanya kazi kwa kuzingatia taaluma na maadili.
hiyo iweze kufanya kazi kwa kuzingatia taaluma na maadili.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia