Monduli.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema jana aliongoza kampeni za Chadema
za udiwani katika Kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli kwa staili ya
aina yake, akitumia helikopta huku ikidondosha vipeperushi vya mgombea
wa chama hicho, Japhet Sironga.
Akizungumza
katika kampeni hizo, Lema alisema: “Chama chetu kina uhakika wa ushindi
kwani Sironga ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Ilboru, ana uwezo
mkubwa kwa kuwa ni msomi.
Lowassa
ndiye aliyepewa mikoba na CCM ya kumnadi mgombea wa chama hicho na
Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wabunge wa chama
hicho Mei 19, mwaka huu Mjini Dodoma alisema kiongozi huyo anatosha
kukipa ushindi katika kata hiyo.
Lema
alisema: “Makuyuni, hamna maji, hamna huduma za afya, hakuna barabara
za vijiji, wafugaji ardhi yenu inaporwa sasa ukombozi wenu umefika kama
mkimchagua msomi Sironga.”
Alimkabidhi
mgombea huyo taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) na kumtaka kazi yake ya kwanza iwe kuibua ufisadi na kumfikishia
bungeni ili kuiokoa Halmashauri ya Monduli.
Akizungumza
katika kampeni hizo, Sironga alisema ameamua kuingia katika
kinyang’anyiro hicho, ili kuokoa jamii ya Makuyuni na Monduli kutokana
na shida zinazowakabili.
ADC Kigamboni
Chama cha ADC kimezindua kampeni ya nyumba kwa nyumba ya uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Mianzini, Kigamboni, Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Kigamboni, Mwenyekiti wa ADC Wilaya
ya Temeke, Salum Sudi alisema kata hiyo inakabiliwa na changamoto
nyingi ikiwamo kero ya maji, barabara, elimu ya msingi na soko, hivyo
wakipewa ridhaa hiyo kero hizo zitakwisha...
Nyongeza na Pamela Chilongola.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia