Mkuu wa wilaya ya Hai akipokea fulana kwa ajili ya mwenge wa Uhuru
kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni ya nguo ya A to Z ya jijini Arusha,Anuj
Shah
Kampuni ya nguo ya A to Z ya Arusha imetoa msaada wa fulana mia tano na
mia tano kwa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ajili ya mbio za mwenge wa
Uhuru mwaka huu.
Mkurugenzi mkuu wa A to Z,Bwana Anuj Shah amekabidhi rasmi fulana hizo kwa mkuu wa wilaya ya Hai,Bwana Novatus Makunga.
Shah ameeleza kuwa kwa kutambua umuhimu wa mbio za mwengi kwa ajili ya mustakabari wa taifa,ndiyo maana ameamua kutoa mchango wake wa fulana.
"Sisi ni wafanyabiashara ambao kuwepo kwa mazingira mazuri ndani ya taifa kunatupa fursa ya kufanya vizuri na mwenge kwa miaka yote umekuwa nyenzo muhimu ya kuwaunganisha Watanzania bila la kujali dini,kabila ama vipato,"alifafanua.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Hai,Bwana Makunga ameeleza kuwa mwenge wa Uhuru utakuwa wilayani humo Jumatano ya wiki hii.
Amesema kuwa katika wilaya ya Hai utapitia miradi nane,ambapo kati ya hiyo mitatu itazinduliwa na miwili itafunguliwa wakati mingine mitatu itawekewa mawe ya msingi.
Amesema kuwa miradi hiyo ina thamani ya shilingi 1,165,781,250 ambapo mchango wa serikali kuu ni shilingi 666,466,000,halmashauri ya wilaya 15,551,450 na nguvu za wananchi ni shilingi 11,033,800 na wahisani shilingi 472,700,000.
Amesema kuwa mbio za mwenge za mwaka huu zimebeba ujumbe unaosema "watanzania ni wamoja" wenye kauli mbiu "Tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zetu za dini,itikadi,rangi na rasilimali"
Makunga ameeleza kuwa mwenge huo utapokelewa katika eneo la Maili sita ukitokea wilayani Moshi.
Amesema kuwa baada ya kuwa wilayani Ha kwa siku nzima siku inayofuata wataukabidhi mwenge katika wilaya ya Siha katika eneo la Lawate.
Picha: Mkuu wa wilaya ya Hai akipokea fulana kwa ajili ya mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni ya nguo ya A to Z ya jijini Arusha,Anuj Shah

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia