BREAKING NEWS

Sunday, May 5, 2013

HII NDIO MUONEKANO MZIMA WA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA LA MTAKATIFU JOSEPH LILILOPO KATIKA KATA YA OLASITI MKOANI ARUSHA MPAKA SASA KUNAMAJERUHI ZAIDI YA 42

Majeruhi wakiwa wamelala chini mara baada ya bomu hilo kulipuka


MTU mmoja ambae hajafahamika jina lake ameuwawa , mtoto mmoja hali yake ni mbaya na y mahututi na wengine zaidi ya 49 wakiwa wamejeruhiwa vibaya katika tukio la kulipuka bomu majira ya saa  4,Asubuhi leo  wakati wa sherehe za ufunguzi  wa kanisa jipya la Mt joseph,la Roman Katoliki, lililopo Olasiti jijini Arusha.

Ufunguzi wa kaisa hilo ulifanywa na balozi wa Vatikan nchini, Fransisko  Padika,aliyekuwa ziarani mkoani Arusha, akiongozana na askofu wa jimbo kuu katoliki , Josephat  lebulu,  na kuhudhuriwa na waumimi wa makanisa ya Roman katoliki yaliyopo jijini Arusha.

Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital z maunt Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi , wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina   Fredirik, Joram  kisera, Novelt  John, Rose  pius, John  James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regina Fredirik, Joram Kisela, Vovalt  John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, .

Wengine ni Lioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim


Mkuu wa mkoa wa  Arusha, Magesa Mulongo ameagiza vyombo vya ulinzi na  usalama mkoani humo kuhakikisha waliohusika kulipua bomu hilo wanatiwa mbaroni mara moja.

Wakati huo huo  jeshi la polisi limelazimika kutumia mabomu kumnusuru  mwendesha boda boda mmoja katika eneo hilo anayedaiwa alimtorosha mtu anayesadikiwa alirusha bomu hilo lililoaangukia mbele ya kanisa hilo na kujeruhi waumini hao.

Taarifa kutoka katika eneo la tukio zimesema kuwa wakati wa tukio hilo walifika watu wawili wakiwa na pikipiki, na kutoa kitu kilichorushwa wakati wa kukatwa utepe wa uzinduzi wa kanisa hilo
 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates