Lango
Kuu la Kuingilia Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara ambapo Makatibu Wakuu
zaidi ya 10 kutoka Wizara mbalimbali wametembelea kujionea hali ya
tishio lililopo la Ziwa Manyara na Maeneo ya Shoroba .
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akitoa neno
la ukaribisho kwa Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali katika kikao
cha Mawasilisho ya Taarifa ya Tishio la kutoweka kwa Ziwa Manyara na
Maeneo ya Shoroba .
Mwenyeji
wa Ziara ya Makatibu Wakuu,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii,Meja Jenerali ,Gaudence Milanzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa
kikao hicho.
Kaimu
Meneja wa Ikolojia katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ,Yustina
Kiwango akifanya Wasilisho la Taarifa kuhusu tishio la kutoweka kwa Ziwa
Manyara,Maeneo ya Shoroba na Mitawanyiko ya Wanyama Tarangire -Manyara
kwa Makatibu Wakuu hao.
Kaimu Meneja wa Ikolojia katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ,Yustina Kiwango akitoa maelezo kwa Makatibu Wakuu hao .
Miongoni
mwa Majengo yaliyokuwa yakitumika kama Vyoo katika Hifadhi ya Taifa ya
Lake Manyara likionekana kuharibika baada ya maji ya Mvua yaliyoambatana
na Mawe zilizonyesha miaka michache iliyopita.
Muonekana
wa majengo mengine yaliyokuwa yakitumika kama vyo kwa wageni
waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara baada ya kuharibika
kutokana na Maji hayo ya Mvua.
Sehemu
ya Ndege ambao ni kivutio kimojawapo kikubwa katika Hifadhi ya Taifa ya
Ziwa Manyara ambao hutegemea pia uwepo wa Maji katika maeneo hayo
ambayo kwa sasa yameanza kukauka kutokana na Uharibifu wa Mazingira
unaofanywa na Binadamu .
Mkuruenzi
Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi (Mwenye kofia)
akiwaonesha Makatibu Wakuu waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa
Manyara maeneo ya Ziwa Manyara ambayo yameanza kukauka.
Eneo
moja wapo la Vivutio vya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara
likionekana kuanza kukauka kutokana na Athari za kimazingira
zinazosababishwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu zikiwemo ,Kilimo
Uchimbaji wa Madini katika maene ya jirani na Ziwa hilo.
Viabda vinavyotumiwa na Wachimbaji wa Madini katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara .
Moja
ya Mtambo unaotumika katika shughuli za Uchimbaji wa madini katika
Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ukiwa umehifadhiwa katika eneo mojawapo
la Uchimbaji.
Maeneo ambayo shughuli za Uchimbaji wa Madini umekuwa ukifanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara .
Kijana
akifanya shughuli ya uchekechaji wa Mchanga katika moja ya mito inayo
peleka maji Ziwa Manyara ,shughuli hi imekuwa ikifanyika kwa lengo la
kujipatia Madini ana ya Dhahabu ,Hata hivyo zoezi hili linatajwa kuwa
moja ya Uharibifu wa Mazingira unaochangia kukauka kwa Ziwa Manyara.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali ,Gaudence Milanzi
akiwanesha baadhi ya Makatibu Wakuu namna ambavyo athari za kimazingira
zimeanza kuonekana katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara .
Baadhi ya Makatibu Wakuu wakitizama kwa mbali Ziwa Manyara.
Makatibu
Wakuu wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Hifadhi za Taifa
(TANAPA) na wa serikali katika mikoa ya Arusha na Manyara mara baada ya
kihitimisha ziara hiyo.