Kikundi cha
waasi wa Alliance of Democratic Forces (ADF) kimetajwa na ripoti maalum
ya uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa kuwa kilihusika na mauaji
ya askari wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na UN, ushahidi uliopatikana unaonyesha ADF ndio
walifanya shambulizi hilo la kushtukiza na kusababisha vifo vya askari
hao waliokuwa wakilinda amani nchini huko Januari 5, mwaka 2018.
Kufuatia
mauaji hayo Katibu Mkuu wa UN aliagiza kufanyika uchunguzi maalumu
ulioongozwa na Katibu Mkuu Msaidizi anayeshughulikia Taasisi za Sheria
na Usalama, Dmitry Titov.
Uchunguzi
huo ulijikita katika mfululizo wa matukio ya mashambulizi dhidi ya
walinda usalama wa UN katika eneo la Beni, jimbo la Kaskazini Kivu, DRC.
Vilevile
timu hiyo maalumu ilipewa jukumu la kuchunguza tukio la shambulizi la
Desemba 7, mwaka jana ambapo walinda usalama 15 wa Tanzania waliuawa
katika kituo chao Semuliki, huku 43 wakijeruhiwa na mmoja mpaka sasa
hajulikani alipo.
Uchunguzi
huo pia umehusisha mashambulizi mawili ya awali dhidi ya walinda usalama
wa Tanzania yaliyotokea karibu na Mamundioma Septemba 16 na Oktoba 7,
2017.
“Timu
maalumu ya uchunguzi ilikamilisha kwa kusema mashambulizi hayo matatu
dhidi ya walinda usalama wa UN yalifanywa kwa mbinu zinazofanana na
kwamba ushahidi wote unaonyesha ADF kuwa ndio waliofanya mashambulizi,”
ilielezwa katika ripoti.
Pia ripoti hiyo iliendelea kusema kuwa, “timu hiyo ilibaini kuwepo pengo kati ya mafunzo ya MONUSCO na Brigade inayoruhusiwa kupigana (FIB), vilevile Munusco haina mpango mahsusi wa kuongeza nguvu na kuwaondoa walinzi wa amani wakati wakishambuliwa.”
Vile vile ilibaini hakuna amri na udhibiti, ukosefu wa uongozi nawawezeshaji muhimu kama wanaanga, wahandisi na intelijensianavyo ni mapungufu ambayo yanatakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa haraka.
Timu hiyo
maalumu ya uchunguzi ambayo iliwaleta pamoja wataalamu wa jeshi na
usalama, wanasiasa na maofisa wa mipango ya vita na maofisa wa juu wa
Tanzania kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ililenga
kutambua mazingira yaliyopelekea mashambulizi hayo, kutathmini hatua za
MONUSCO na kubainisha hatua zinazotakiwa kuchukuliwa ili kuzuia
mashambulizi yasitokee siku za usoni.