Na Woinde Shizza,
Kondoa
Mkuu wa wilaya ya Kondoa Sezaria Makota Ametoa Agizo kwa
Mamlaka za Serikali zilizo chini yake kuhakikisha mkurugenzi wa Kampuni ya Kidee
Minning Fei Hassan Kidee kumfuata popote alipo iwe nje au ndani ya nchi
kutokana na kukaidi wito wake wa kuhudhuria kikao cha mgogoro katika machimbo
ya dhahabu yalipo kijiji cha bubu changaa.
Hayo yamejiri kwenye kikao cha kujadili mgogoro kati ya
Kampuni za Kidee Mining,Kondoa Mining T ltd na wachimbaji wadogo kwenye
machimbo yaliopo kata ya changaa wilayani hapa
baada ya meneja wa Kampuni hiyo Ismail Kidee kusema mkurugenzi wake yupo
safari nje ya nchi na kushindwa kuhudhuria kikao hicho kujibu tuhuma mbali
mbali.
Amesema kuwa Suala la kuwataka Fei Hassan na Afisa madini
mkazi Dodoma Silimu Tegalile ni Agizo kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa
sheria Anatoa agizo kwa hao kufika kwenye kikao cha Tar.1 mwezi wa 3 mwaka huu
saa 3 asubuhi katika ofisi za kijiji cha Bubu Changaa bila kukosa ili aeweze
kujiridhisha na masuala mbali mbali kwani wao imeonekana ndio chanzo cha
mgogoro huo.
Kampuni hiyo imekuwa ikituhumiwa kwa ukwepaji wa mapato na
kutumia njia za hila kumiliki Eneo la machimbo ya dhahabu wilayani hapa kwa
madai wao wamepewa fursa ya utafiti wa madini kwenye wilaya ya Kondoa ambapo
wachimbaji wamekuwa wakinyang’anywa maeneo yao licha ya maombi halali kwenye
idara za madini uliofanywa na wachimbaji hao na upotoshwaji wa Taarifa kwani
maombi hayapewi majibu kama sheria inavyosema.
Mgogoro huo uliodumu kwa muda wa mwaka mmoja sasa huku
mamlaka mbali mbali za serikali zikishindwa kutoa tafsiri ya nani mmiliki
halali wa eneo hilo ambapo kampuni hiyo imesema ina leseni huku wizara ikisema
eneo hilo maombi yote yalipishana na leseni kubwa iliyopelekea kutotolewa kwa
leseni za uchimbaji na utafiti eneo la bubu changaa na hiyo ndio imeleta
sintofahamu ambayo Kamishina wa kanda ya kati na idara ya madini mkazi Dodoma
imeshindwa kutoa tafsiri mwaka sasa na kuendelea kulifumbia macho bila majibu.
Hali hiyo imekuwa ikiwasumbua wachimbaji wadogo kutoendelea
na utafiti wao kwa madai ya leseni na kuwafanya kushindwa kutimiza malengo yao
na kijiji kukosa maendeleo kwa mwaka mzima kwa uzalishaji wa wachimbaji hao
ungekuwa na manufaa kwa wananchi ili hali akilazimisha kupitia ofisi za madini
kufanyakazi katika eneo hilo na kubaka eneo la wachimbaji hao huku wachimbaji
wakilalalikia uainishwaji wa mipaka ya leseni za uchimbaji na matumizi bora ya
Ardhi katika eneo hilo.
“Nakuagiza kwa
mamlaka niyopewa dso na idara ya uhamiaji kulifuatilia suala hili kuona kama
mkurugenzi huyo amepiga mhuri wa kutoka nje ya nchi au yupo hapa nchi na
amekaidi agizo lango kwa maksudi atafutwe aletwe popote alipo kwani hatuwezi
kuona tunamuita kwenye vikao vya kutafuta suluhu yeye anatuma wawakilishi hii
ni dharau ya wazi” alisisitiza Dc Makota.
Awali akifungua na kufunga kikao hicho mwenyekiti wa Kijiji cha Bubu Changaa
Kenyata Fonda alisema kuwa suala hilo limekuwa ni changamoto kwa wananchi kukua
kiuchumi na kijiji chake kwa ujumla kukosa maendeleo na kumuomba mkuu huyo wa
wilaya kuhakikisha mgogoro huo unaisha mapema ili wanachi waweze kufanya
shughuli zao za kujipatia kipato.
Amesema kuwa Suala hilo wananchi wanataka maendeleo lakini
hawayapati kutokana na mgogoro huo nadhani katika mgogoro huo kuna kitu
kimejificha ndani naiomba serikali kuingilia kati kuona wananchi wanapata
maendeleo kutokana na rasilimali za eneo lao.