Mjumbe wa halmashauri kuu ya
taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha
jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi
milioni sita (6,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Mufindi kwa kutoa kiasi cha
shilingi milioni sita kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana
kuwa tegemezi. Mjumbe wa halmashauri kuu ya
taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akikabidhiwa shati na umoja wa wanawake (UWT) wilaya ya Mufindi baada ya kukabidhiwa kofia ambayo ameifaa hapo
Mjumbe wa halmashauri kuu ya
taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akifurahia jambo na viongozi wa chama hicho pamoja na wabunge wa viti maalum mkoa wa Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MJUMBE wa halmashauri kuu ya
taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha
jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi
milioni sita (6,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Mufindi kwa kutoa kiasi cha
shilingi milioni sita kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana
kuwa tegemezi.
Pesa hizo zimetolewa wakati wa
baraza la umoja wa wanawake wilaya ya Mufindi mkoani (UWT) lilofanyika katika
ukumbi wa chama cha mapinduzi ulipo mjini Mafinga na kuhudhuriwa na wageni wengi
wakiwepo wabunge wa viti maalum ambao ni Ritta Kabati,Rose Tweve na mama
Mwamwindi.
Akizungumza katika baraza hilo
MNEC Asas alisema kuwa amependezwa na mikakati ambayo imefanya na umoja huo wa
wilaya ya mufindi kwa kuwa wanafanya kazi na viongozi pamoja na wananchi wa
chini hivyo inakuwa rahisi kuendelea kukijenga chama hicho.
Nimeona kwenye hotuba yenu
mmesema kuwa “mtahakikisha kuwa wanawake wanajiunga kwenye vikundi vya
uzalishaji kama vile vikoba ,saccos na vikundi vingine ili waweze kupata mafunzo
stahiki ya ujasiliamali kwa lengo la kupambana na hali ya kiuchumi na kuongeza
kipato,”hakika kwa kufanya hivi mtawaokoa wanawake wengi sana kiuchumi. Alisema
Asas
Asas alisema kuwa nimesikia
mnataka kujenga kipanda kwa ajili ya kuongeza ajira na kuongeza uchumi wa umoja
huu,hilo ni jambo bora hivyo kwa kuona mikakati hiyo nawachangia kiasi cha
shilingi milioni sita ili mfikie malengo yenu.
“Sijaona changamoto ila nimeona
matarajio ambayo ni kuanzisha mradi wa kuuza sare za chama,kumalizia ujenzi wa
vibanda vya umoja wenu,kutafuta eneo la ekar 5 kwa ajili ya kilimo cha viazi na
kupanda miche ya miparachichi na kutafuta kiwanja kikubwa kwa ajili ya
uwekezaji na ndio sababu iliyonifanya niwachangie kiasi hicho cha pesa” alisema
Asas
Aidha Asas alimpongeza mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Twelve
kwa jitihada alizozifanya za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoa
mitaji kwenye kata kumi na saba kwa
kutoa kiasi cha silingi laki sita kwa kila kata,hivyo kwa kuliona hilo MNEC
alisema kuwa atachangia kiasi cha shilingi laki tano kwa kila kata kwa kata
zote 36 za wilaya ya Mufindi.
Kwa hili sipepesi macho
nampongeza sana mbunge Rose Tweve kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha
wanawake wanapata mafanikio kwa kuwawezesha kama alivyofanya kwa kufanya hivyo
amefanikiwa kuwafikia wanawake walio na kipatao cha chini kabisa na nitaendelea
kukusaidia mbunge kwa kazi unazozifanya kwa ajili ya maendeleo” alisema Asas
Kwa upande wake katibu wa UWT
wilaya ya Mufindi Mwanaidi Kaleghela alimshikuru MNEC Salim Asas kwa kutoa
msaada mkubwa kama huo ambao hata wao hawakutegemea kutokea kitu kama
hicho,ukipiga mahesabu utagundua kuwa ametoa milioni ishirini na nne kwa UWT
mufindi.
“Ametoa shilingi mioni sita kwa
UWT na ametoa milioni kumi na nane kwa ajili ya kuongezea nguvu kwenye mfuko wa
mbunge Rose Tweve hivyo lazima tujivunie kuwa na MNEC wa namna hii” alisema Kaleghela