Shirika lisilo la kiserikali la Tumaini Jipya lenye makazi yake
kata ya Olkokola halmashauri ya Arusha limeonesha kuridhishwa na
utekelezaji wa shughuli za kuwahudumia wananchi zinazofanya na
halmashauri hiyo tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza kwa njia ya mtandao mkurugenzi na mwanzilishi wa shirika
hilo Bi. Louise Richardson raia wa Uingereza amesema kuwa ameridhishwa
na utekeleza shughuli za kuwahudumia wananchi katika halmshauri ya
Arusha kwa ili kutatua changamoto za huduma za kijamii zinazowakabili
wananchi hasa wa maeneo ya vijijini.
Louise ameoneshwa kuridhishwa zaidi na utekelezaji wa mradi wa maji
wa vijiji vitano mradi ambo yeye binafsi ndiye chanzo cha upatikani wa
ufadhili wa mradi huo kutoka nchini kwake Uingereza, baada ya kushuhudia
adha ya maji wanaipata hasa watoto wakike wawapo shuleni na kuamua
kurudi nchini kwao kutafuta fedha za kutekeleza mradi wa maji.
Hata hivyo Louise amesema hayo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa
mkuu wa Kitengo cha huduma ya Jamii 'DFID' Bi. Getrude Mapunda
aliyetembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo wa maji
mwishoni mwa wiki iliyopita, ameanza kuona upatikanaji wa huduma ya maji
katika vijiji hivyo ambavyo kiuhalisia wana shida kubwa ya upatikani wa
maji safi na salama.
Amesisistiza kuwa lengo hasa la shirika la Tumaini Jipya ni
kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kuhakikisha
huduma zote za jamii zinawafikia wananchi hasa waishio vijijini na
kufafanua kuwa endapo mradi huo utatekelezwa kwa wakati na kwa viwango
na jamii kushiriki katika utunzaji na uchangiaji wa huduma za maji ili
huduma hizo ziwe endelevu, serikali ya Uingereza itaendelea kutoa
misaada mingi kupitia shirika lake la Tumaini Jipya.
Shirika la Tumaini Jipya limekuwa likifadhili shughuli mbalimbali za
maendeleo ikiwemo uwekaji vioo kwenye vyumba vya madarasa shule ya
msingi Olbaki pamoja na kweka miundombinu ya umeme kwenye nyumba za
walimu wa shule hiyo pamoja na zahanati ya kijiji cha Lengijave .
Licha ya misaada hiyo Louise ametoa msaada wa mashine ya kusaga
nafaka ili kutatua changamoto inayowakabili wakazi wa kijiji cha
Lengijave ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo, mradi huo
utakaoanza kufanya kazi mara baada ya mchakato wa kuingiza umeme
kukamilika.
Hata hivyo Louse amesema kuwa shirika la Tumaini Jiya liko tayari
kuendelea kutoa misaada mbalimbali ya kijamii kwenye sekta za elimu,
afya na maji nchini Tanzania kutokana na mapenzi mema aliyonayo hasa kwa
wananchi wa kijiji cha Lengijave eneo ambalo amewahi kuishi kama
'volontia'.
Bi. Louise ambaye ni Diwani nchini Uingereza, ndiye chimbuko hasa la
mradi wa maji wa vijiji vitano baada ya kukerwa na changamoto ya ukosefu
wa maji hasa kwa watoto wakike wawapo shuleni na kuamua kurudi nchini
kwao kutafuta fedha, Mradi wa maji wa vijiji vitano unafadhiliwa na
serikali ya Uingereza kupitia wa na Idara ya Maendeleo ya kimataifa
'DFID' na kutekelezwa na shirika la WaterAid- Tanzania.