Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
kimemsimamisha kuendelea na masomo mwanafunzi wake wa mwaka wa tatu, Abdul
Nondo baada ya kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa
Nondo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa
Wanafunzi Tanzania (TSNP), amesimamishwa kuanzia Machi 26, 2018 kwa barua
iliyoandikwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye
Akizungumza leo na Mwananchi Machi 27, 2018,
Profesa Anangisye amesema, “ni kweli barua ya kumsimamisha ni yangu na
tumefanya hivyo kwa mujibu wa tararibu zetu
Profesa Anangisye amesema mwanafunzi
anapokuwa amepandishwa kizimbani na akawa na kesi ya kujibu husimamishwa na
akishamaliza kesi yake anarejea kuendelea na masomo
Wakili wa mwanafunzi huyo, Jebra Kambole amesema
kuwa mpaka sasa mteja wake hajapata barua hiyo
“Hatujaipata na hata Nondo mwenyewe pia
hajaipata na wala hatujui chochote kuhusu suala hilo hivyo siwezi kusema kama
ni ya kweli au ndio mambo ya kwenye mitandao. Ila pia kama ni kweli kwanini
isambae mitandaoni, inapaswa apewe mwanafunzi mwenyewe,” amesema