Wanawake wa Arusha watakiwa kutumia vizuri mikopo yao kwa kuwekeza
kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo na zitakazo zalisha kwa wingi
na kuwaletea mapato yakutosha katika familia zao.
Ameyasema hayo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri
Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Jenista Muhagama
alipokuwa akikabizi hundi ya milioni 120 ya mkopo wa akinamama
wajasiliamali, Jiji la Arusha.
Amewataka wanawake waonyeshe kuwa wanaweza kuinuka kiuchumi na kuacha
utegemezi huku wakitekeleza majukumu yao katika ngazi za familia na
jamii kwa ujumla.
“Mikopo hiyo mnayoenda kupewa ichukulieni kama mmepata tunda la embe
katika mti wa miba,yani haitakaa itokee tena mkapatiwa mikopo hiyo kwa
mara nyingine”.alisema
Aidha,amewahasa wakatumie vizuri mikopo hiyo na waache kwenda
kununua vitu ambavyo havitawasaidia katika kujiletea maendelea yao na
familia zao.
Serikali ya awamu ya tano imelenga katika kuhakikisha matunda ya nchi
yanaliwa na kila mtanzania,hivyo fursa hiyo ya wanawake kupatiwa mitaji
kwa mikopo isiyo na riba nimkakati mzuri wakutelekeza ilani ya chama
cha mapinduzi.
Amesema wizara yake ipo tayari kuwasaidia wakimama wote watakao
fanikiwa kumaliza marejesho yao na atawasaidia kupata mikopo mingine ya
riba nafuu huku wakiwa katika vikundi.
Pamoja na akimama kipatiwa hiyo mikopo wanaweza pia kutafuta fursa
kubwa zaidi katika miradi mikubwa inayofanywa na serikali,ili na wao
waweze kukua katika biashara zao.
Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa juhudi alizozifanya za kusaida
makundi maalumu ya vijana,wanawake na wenye ulemevu katika
kuwatengenezea ajira zaidi ya 200.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema akinamama ni kundi kubwa
sana linalotegemewa kwa asilimia kubwa katika ngazi za familia na jamii
kwa ujumla,hivyo aliona hana budi kutafuta namna yakuwawezesha ili
waweze kujikwamua katika maisha yao.
Amewataka wenye mapenzi mema waendelee kusaidia akinamama katika
Nyanja ya kujikwamua kiuchumi ile pale wanapokosa usaidizi basi waweze
kusimama wao kama wao na kuendesha maisha yao na wategemezi wao.
Akisisitiza zaidi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,amesema
mwanamke nisawa na hewa ya oxjeni pale inapokosekana inaleta maafa
makubwa na pengine kupoteza kabisa uhai wa binadamu.
Akitoa salamu za pongezi Mwenyekiti wa Tanzania Tour Operators
(TATO) bwana Wilbad Chambulo kama mmoja wa wadau amesema alichofanya
Gambo ni jambo la kuigwa na watu wengine na yeye atachangia kiasi cha
milioni 20 ili wakimama wengine 100 waweze kukopeshwa.
Mikopo isiyokuwa na riba ya kuwezesha makundi mbalimbali katika Mkoa
wa Arusha ilianza kwa vijana 200 kukopeshwa pikipiki na baada ya kufanya
marejesho yao kiasi cha milioni 120 kimetolewa kuwakopesha akinamama
600 kama mtaji wakufanya biashara mbalimbali.