Halmashauri ya Wilaya ya Meru inamiliki mitambo ya kutengeneza
barabara ambayo ni Motor Grader na Soil Compactor(Roller) ambayo
hutumika kama chanzo cha mapato.
Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Emmanueli G.Joram
amesema ukodishaji huo wa mitambo ya kutengeneza barabara utaiwezesha
Halmashauri ya Wilaya ya Meru kupata mapato ya ndani ambayo asilimia 60
ya mapato hayo itatumika kutekeleza shughuli za maendeleo na kutoa
huduma bora kwa wananchi kwani kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri
hiyo kupitia Mkutano wa baraza lake imepitisha mpango wa bajeti kiasi
cha Tsh 57,137,649,851.60 ikiwa Tsh. 4,000,000,000.00 zinatokana na
mapato ya ndani(own source) na Tsh.53,137,649,851.60 ni fedha kutoka
serikali kuu .
.