Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo amewaonya vikali wakuu
wa idara mbalimbali za serikali ambao hawafanyi kazi zao kwa weledi hadi
kusubilia ukaguzi wa viongozi wakuu.
Gambo amesema hayo wakati akiutimisha ziara yake ya siku ya kwanza
ya ukaguzi wa ujenzi wa viwanda vipya jijini Arusha katika kiwanda cha
MONABAN TRADING COMPANY LTD cha utengenezaji wa mifuko kilichopo katika
kata ya moshono jijini Arusha.
Gambo ameeleza kwamba kumekuwa na uzembe mkubwa wa watendaji wa
serikali hasa wakuu wa vitengo kutowafuata wawekezaji kujua changamoto
zao hadi pale viongozi watakapo fanya ziara katika maeneo mbalimbali
kwaajili ya ukaguzi wa maendeleo na watumishi hao kutokuwa na majibu ya
kutosheleza kutokana na kujifungia maofisini na sio kufanya kazi za
wananchi.
Aidha pia Gambo amemuagiza Katibu Tawala wa mkoa Richard Kwitega
kuwafuatilia kwa ukaribu watendaji hao ili kuacha kufanya kazi kwa
mazoea kwani hivi sasa ni zama za utendaji kazi na sio zama za kulala na
kuwataka kama hawawezi kwenda na kasi ya Dk Magufuli waache kazi mara
moja na kuwapisha watu wenyeuwezo.
"Nikutake katibu mkuu wa mkoa kuwafatilia kwa karibu sana watendaji
wazembe wanao fanya kwa mazoea waache mara moja kwani hawamu ya tano ni
ya utendaji kazi na inamalengo ya kufikia uchumi wa kati na Tanzania ya
viwanda sitaki mzaa katika kazi na nitaakikisha ninakaa na taasisi zote
za serikali kama Tanesco, TRA , TANROAD,TARURA pamoja na AUWASA ili
kuahikisha changamoto zite zinazo wakabili tunazimaliza." Alisema Gambo.
Aidha Mrisho Gambo aliwahakikishia wawekezaji wote wa jiji la
Arusha kuwa serikali ya awamu ya tano ipo tayari kuwapokea na kuwajali
kani dhumuni la serikali ni Tanzania ya viwanda na kuwataka waweke
kipaumbele kuwaajili watanzania na kuwapongeza wakezaji hao kwa ujasili
na ukomavu wa kuweza ndani ya wa muwekezaji wa kiwanda cha MONABANI
TRADING COMPANY LTD, Ndg Philemon Mollel ( MONABANI ), ameweza kuiomba
serikali kupunguza kodi za tozo kwa kuagiza malighafi nje ya nchi kwa
ajili ya utengenezaji mifuko hiyo hapo kiwandani ili kuweza kumudu
gharama za uwekezaji.
"Nikuombe mkuu wa mkoa kutufikishie changamoto zetu za ukubwa wa
kodi zinatufanya tushindwe kuwekeza na kuendesha viwanda ndani ya nchi
tuiombe serikali utufikilie upya katika tozo ili tuweze kuendana na
kaulimbiu ya serikali ya viwanda" Alisema Mollel.
Awali akisoma lisara ya ujenzi wa kiwanda mkurugenzi wa fedha wa
kampuni hiyo Nathan Mollel ameeleza kuwa hadi kukamilika kwa kiwanda
hicho kitaghalimu jumla shilingi Bilioni 9.6 na na kitakuwa na uwezo wa
kuzalisha jumla ya mifuko milioni moja kwa mwaka huku kikiwa kimetoa
ajira kwa watanzania wasio pungua 150.
Ziara hiyo ya mkuu wa mkoa iliyoa anza leo ya kutembele viwanda nane
vipya vinavyo jengwa katika jiji la Arusha na inategemewa kumalizika
tarehe March 23 mwaka huu ambapo anatembelea viwanda vya Athere to ideal
making Ltd, The Old Moshi Distillery Ltd pamoja na Monaban Trading and
Compay Ltd,Tanzania Geomolohical Cetre, International Dairy
Product,Bhuni Mbuni Co.Ltd, Swed Tan Ltd pamoja na Sterling Surfactants
Ziara hiyo ya ukaguzi wa viwanda imeanza baada ya Rais wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ya kuwataka wakuu wa
mikoa yote kuhakikisha kila mkoa unakuwa na viwanda 100 mpaka ifikapo
mwisho wa mwaka huu.