Serikali yajipanga kupokea mradi wa Global Learning XPRIZE

Serikali imesema inajiandaa kuupokea mradi wa ‘Global Learning XPRIZE’ unaowawezesha watoto walio nje ya mfumo rasmi kujifunza stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kupitia Michezo iliyowekwa kwenye tableti, kutoka kwa wadau wanaoufadhili baada ya kumalizika muda wa majaribio. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi kutoka TAMISEMI anayeshughulikia elimu nje ya mfumo rasmi na Elimu ya Watu Wazima, Odilia Mushi wakati akizungumza katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na taasisi mbalimbali za serikali.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka TAMISEMI anayeshughulikia elimu nje ya mfumo rasmi na Elimu ya Watu Wazima, Odilia Mushi akizungumza kuhusu maandalizi ya serikali kuupokea mradi wa Global Learning XPRIZE.
Kama serikali mradi unapomalizika tunaangalia namna ya kuuendeleza. Tutaendelea kushirikiana na halmashauri zetu zilizoko kwenye mradi wauone kama ni wa kwao na kwamba badala ya watoto kuzurura mitaani wanaendelea kujifunza,” amesema Mushi na kuongeza. “Tunaagiza wale wahusika, wadau wa elimu katika ngazi zote za kijiji hadi mkoa wa Tanga waone kama hiki kilicholetwa kwetu ni zawadi,na ni lazima kuuendeleza ili kupunguza watoto walioko nje ya mfumo rasmi; kwa maana hiyo inatakiwa tuwe na ushirikiano kuona changamoto baada ya huu mradi kumalizika ili kuzifanyia kazi.”
Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akizungumza kuhusu mradi wa Global Learning XPRIZE.
Akielezea utekelezaji wa mradi huo tangu ulipoanza na ulipofikia, Afisa Msaidizi wa Mradi kutoka UNESCO, amesema hadi sasa watoto zaidi ya 2000 kutoka vitongoji 141 katika wilaya 6 za mkoa wa Tanga wamenufaika na mradi huo. “Baada ya miezi 15 ya mradi kukamilika, mradi utakabidhiwa kwa serikali ili kuendelea kuusimamia. , ambapo tumekutana leo Tarehe 13/3/2018 na wawakilishi kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (BMT) , Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na TAMISEMI ili kuweza kuangalia ni jinsi gani watoto walio katika mradi wataingia katika mfumo rasmi katika ngazi husika,” amesema.
Wadau mbalimbali wakichangia katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na taasisi mbalimbali za serikali kuhusu mradi wa Global Learning XPRIZE.

Washiriki wa mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na taasisi mbalimbali za serikali kuhusu mradi wa Global Learning XPRIZE.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post