Vijana nchini wametakiwa kutumia vizuri na kwa ungalifu mitandao ya
kijamii, itumike hasa katika kujipatia elimu mbalimbali zakuwajenga na
kuleta maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Dokta Harrison Mwakyembe alipotembele kituo cha redio cha Sunrise
nakukutana na uongozi na wafanyakazi wa kituo hicho.
Amesema tayari sheria ya mtandao na kanuni zake ipo kwenye hatua za
mwisho, hivyo amewataka watumiaji wa mitandao hiyo kuwa makini sana
kwani sheria itakapoaanza haita mwacho yoyote ambae ataikiuka.
Nchi nyingi zinatumia hii sheria na Tanzania tulichelewa kuanza
kuitumia,hivyo niwakati sasa wakuhakikisha maadili ya nchi yanazingatiwa
na kufuatwa.
Pia amevitaka vyombo vya habari kufanya kazi kwa kufuata sheria na
maadili ya nchi, ili kujenga vizazi vyenye kufanya kazi kwa weredi na
heshima.
Aidha,amesema serikali inafanya kazi na vyombo vya habari kwa kufuata
sheria ya uhuru wa habari, hivyo penye kutoa taarifa zinazowahusu
wananchi itafanya hivyo ili wananchi waweze kufahamu kwa kina mambo yote
yanayoendelea katika serikali yao.
Serikali ipo tayari kupokea taarifa yoyote inayokosoa kwenye mambo
mbalimbali ya maendeleo na kuweza kuifanyia kazi, ili kuleta maendeleo
ya nchi kwa ujumla.
Hata hivyo amesema, serikali haitafumbia macho chombo chochote cha
habari kitakacho toa taarifa za uwongo na uchochezi,hivyo sheria
itachukua mkondo wake.
Amesisitiza zaidi kwa wananchi wa Arusha kujifunza jinsi yakuboresha
ujasiliamali ili uwe wakuwanufaisha hususani fursa za utalii na nyingine
nyingi.
Dokta Mwakyembe yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku 3
ambapo atafungua mkutano wa Maafisa Habari nchini,atatembelea na kukagua
uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid na atazungumza na wadau wa
utamaduni,sanaa na michezo.