Ticker

6/recent/ticker-posts

THE GRANDE DEMAM KIWANDA CHA MAZIWA KINACHOWANUFAISHA KIUCHUMI WAFUGAJI 2000



 Baadhi ya Wafanyakazi na Viongozi wa Kiwanda cha Maziwa cha The Grande Demam wakihakiki ufungashaji wa bidhaa za maziwa zinazozalishwa kiwandani hapo
Baadhi ya Viongozi wa kiwanda cha maziwa cha  The Grande Demam wakinywa maziwa yanayozalishwa na kiwanda hicho
 Baadhi ya Viongozi wa kiwanda cha maziwa cha  The Grande Demam wakinywa maziwa yanayozalishwa na kiwanda hicho
Uongozi wa kiwanda cha maziwa cha  The Grande Demam

Na Woinde Shizza ,Arusha.
Wilaya ya Meru ni moja kati ya Wilaya maarufu zinazoongoza kwa uzalishaji mkubwa wa maziwa mkoani Arusha,maziwa ambayo huuzwa maeneo ya miji ikiwemo viunga vya Jiji la Arusha na nje ya jiji hilo.

Licha ya uzalishaji huo wa maziwa bado wafugaji hao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa masoko ya uhakika ya kununua maziwa hayo hivyo kupelekea maziwa wanayoyazalisha kuharibika baada ya kukaa muda bila kununuliwa.

Kufuatia Changamoto  hiyo  Moja kati Daktari wa Mifugo Dokta Deo aliona changamoto hiyo kama fursa ya uwekezaji kwani malighafi ya maziwa inapatikana kwa wingi ,kwa kuwa wafugaji walikua wakiyamwaga maziwa yao yaliyokua yakiharibika kwa kukosa soko la uhakika  na hawakua na namna yoyote ya kuongeza thamani maziwa hayo ili yaweze kukaa kwa muda bila kuharibika.

Dokta Deo aliacha kazi ya kuajiriwa mwaka 2001 na kuamua kufuga ng`ombe 1  baadae  wawili ambao walikua wakitoa  lita 40 kila siku huku yeye na familia yake wakitumia lita 1 hivyo maziwa mengine kuharibika baada ya kukaa kwa muda.

Suala hili lilimfikirisha sana Dokta Deo ambaye alimtafuta mtaalamu kutoka nchini Kenya  atakayemfundisha jinsi ya kuongeza thamani maziwa yake ,kuyafungasha na kuyauza .Mtaalamu huyo alimfundisha ndipo akaianza kazi ya kuongeza thamani maziwa hayo nyumbani kwake.

Baada ya muda majirani zake wafugaji walianza kuvutiwa na jinsi anavyoongeza thamani maziwa yake na walimletea maziwa ili ayaongeze thamani ndipo alipoanza kununua maziwa na kuongeza thamani takribani lita 100,150 mpaka 200 kwa siku.
Baada ya hapo akafungua kiwanda kidogo ambacho kilikua na uwezo wa kusindika lita 200  kwa siku huku wafugaji wakileta maziwa  mengi zaidi  ndipo alipoongeza uzalishaji na kwa sasa anazalisha lita 2000 kwa siku.

Kutokana na ongezeko hilo lauzalishaji kwa sasa Dokta Deo pamoja na Wakurugenzi wenzake wa kiwanda hicho cha The Grande Demam wameongeza wigo na kununua maziwa zaidi kwa wafugaji ambao walikua wakiteseka kupata masoko na wakati mwingine kumwaga maziwa yao yanayoharibika kwa kukaa muda mrefu bila kununuliwa.

Kiwanda hicho kinanunua maziwa bora kutoka kwa wafugaji na kuyaongezea thamani ikiwa ni pamoja na kuyafungasha vyema.

“Maziwa ambayo hayajaongezwa thamani hukaa kwa muda wa masaa 13 lakini maziwa yaliyoongezwa thamani yanaweza kukaa hadi mwezi mmoja jambo ambalo linaleta unafuu hasa kwa kipindi kifupi kabla hayajafika sokoni” Alisema Dokta Deo


Dokta Deo anaeleza kuwa maziwa yaliyosindwa ni maziwa mazuri kwa afya ya binadamu yamekua yameondolewa bacteria hatarishi na kuongezewa bacteria rafiki kwa afya.

Mtu anayetumia Maziwa ambayo hayajasindikwa anakua yuko hatarini kupata magonjwa mbalimbali ikiwemo Tb,Typhoid na Brusela.

Pia maziwa yaliyosindikwa kiwandani yanasaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yanayoweza kuambukizwa kutoka wanyama kwenda kwa binadamu.

Mkurugenzi wa kiwanda hicho Dokta Deo amesema kuwa maziwa ni bidhaa yenye faida kubwa sana katika mwili wa binadamu ikiwemo virutubisho aina ya Protini,Madini,Fat pamoja na wanga.

Dokta Deo anashauri unywaji wa maziwa uhamasishwe kwa wingi katika jamii ili kuwa na jamii yenye afya bora inayoweza kushiriki katika shughuli za uzalishaji.

Anaeleza kutokana na ubora wa maziwa yanayozalishwa na kiwanda hicho wateja wamekua wakiyafurahia hivyo wanafirikiria kuongeza uzalishaji na kuboresha zaidi ili kuwafikia wateja wengi zaidi.

“Tuna mpango wa kuzalisha mpaka lita laki moja kwa siku ,uzalishaji huu utaleta tija kwa kiwanda pamoja wafugaji ambao tumekua tukinunua maziwa kwao tutanunua maziwa mengi zaidi hivyo kukuza kipato cha wafugaji waweze kunufaika na shughuli zao za ufugaji” Alisema Dokta Deo

Ni vyema Watanzania wakajifunza kunywa maziwa  haya bora yanayozalishwa nchini badala ya kunywa maziwa kutoka nje kwani kwa kufanya hivyo utakua unainua uchumi wa nje.


Biashara hiyo ya maziwa imesaidia vijana wengi  waliojiriwa na kiwanda hicho katika sekta ya uzalishaji na usambazaji jambo ambalo linaonyesha mnyororo wa wanufaika wa kiwanda hicho unavyoongezeka.

Kwa sasa  bidhaa za maziwa,Yogat na Siagi za The Grande Demam imefika katika mikoa ya Dar es Salaam ,Manyara ,Tanga na Morogoro.


Mshauri wa  Masuala ya Biashara katika Kiwanda Peter Ojukwu  hicho amesema kuwa kiwanda hicho kinaweza kuwanufaisha watu zaidi ya 4500 kutokana na mzunguko wa uzalishaji mpaka kumfikia mlaji.

Anaeleza kuwa licha ya kiwanda hicho kujikita na uzalishaji wa maziwa bado kinatoa huduma za ushauri wa ufugaji bora,matibabu ya mifugo pamoja na madawa ili waweze kufanya ufugaji wenye tija.

Pia anashauri serikali na taasisi binafsi kuunga mkono juhudi za Wawekezaji wanaowekeza kwenye viwanda ikiwamo kiwanda cha maziwa kwani kinagusa maisha ya watu wengi moja kwa moja.

“Kama unavyojua katika maziwa hakuna kinachosalia unatoa maziwa,siagi,yogati,samli,mtindi  hivyo hakuna kinachotupwa kila kitu kina thamani kubwa” alisema Mshauri huyo

Nassari na ni moja kati ya Wafugaji ambao maziwa yao yananunuliwa na kiwanda hicho wamesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kiwanda hicho wamekua wakipata soko la uhakika la maziwa yao hivyo kuondokana na tatizo la maziwa kuharibika  kwa kukosa soko.

Anaeleza kuwa uwepo wa kiwanda hicho umewasaidia wafugaji wengi ambao walikua hawana pa kuyapeleka maziwa yao lakini kwa sasa wanafika katika kiwanda hicho na kuyapeleka maziwa yao.

Post a Comment

0 Comments