Naibu
waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati
akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyang'wale
iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hivyo Mhe Hamim Gwiyama akiwa katika
ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Naibu
waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisalimiana na baadhi ya
watendaji katika Wilaya ya Nyang'wale mara baada ya kuzuru wilayani
Nang'wale akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018.
Kamati
ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyang'wale iliyoongozwa na Mkuu wa
Wilaya hivyo Mhe Hamim Gwiyama ikimsikiliza kwa makini Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018.
Naibu
waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (aliyesimama) akielezea
mikakati ya wizara hiyo wakati alipozuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Nyang'wale akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018, Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale Mhe Hussein Nassor Amari Kasu, na Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Mhe Hamim Gwiyama
Na Mathias Canal, Geita
Serikali
ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli tangu ianze utendaji wake
imejipambanua wazi kuwa rasilimali zote za nchi ikiwemo madini ni muhimu
sana kwa maendeleo ya Taifa hivyo ni Mali ya watanzania wenyewe sio
wawekezaji wa kigeni.
Baba
wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusisitiza
kuwa katika rasilimali Madini Taifa halipaswi kukurupuka kuyachimba kwa
kuwa uwezo wa kitaaluma na kiteknolojia kuwezesha kuyachimba na
kuyafaidi kama Taifa ulikuwa mdogo kwa mantiki hiyo, Baba wa Taifa
akaenda mbali zaidi kwa kuagiza madini yasichimbwe hadi hapo Taifa
litakapokuwa na uwezo wa kuyachimba ili watanzania waweze kunufaika
ipasavyo.
Hayo
yamebainishwa na Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko Leo 6
Machi 2018 wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya
ya Nyang'wale iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hivyo Mhe Hamim Gwiyama
akiwa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita.
Mhe
Biteko alisema kuwa Mwalimu kwa wakati huo alijua fika kuwa Tanzani a
ikifungua milango ya kuchimba madini bila Taifa kujenga uwezo imara wa
kufanikisha lengo hilo ipasavyo, wataalamu na wafanyabiashara au wale
wanaoitwa wawekezaji kutoka nje, ilimradi wanazo fedha nyingi;
watalilalia Taifa na kuwadanganya watanzania na hatimaye kuweza
kufaidika zaidi kutokana na rasilimali madini.
Alisema
kuwa Kwa mtazamo huo Rais Magufuli, aliamua kuweka mbele utaifa kuliko
maslahi binafsi kwa kuifufua sheria ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa
mabadiliko mwaka 2017 ili kuiyafanya rasilimali Madini kuwa na manufaa
kwa watanzania wenyewe kuliko ilivyokuwa awali.
"Mimi
nataka niwaambie kuwa rasilimali madini ni mali ya Taifa letu au kwa
maneno mengine ni mali ya Watanzania; na viongozi (kwa ngazi zote)
tumepewa dhamana tu ya kusimamia na kuhakikisha Taifa letu linanufaika
kutokana na uchimbaji madini, na si vinginevyo" Alisema Biteko
Aliongeza
kuwa Taifa linaweza kuendelea zaidi endapo kwa wachimbaji kwa pamoja
watakubali kufuata sheria na taratibu za uchimbaji huku wakiunga mkono
juhudi za serikali kwa kulipa kodi ili kuwa na mafanikio wezeshi kwa
watanzania wote.
Kwa
upande wake Mbunge Wa Jimbo la Nyang'wale Mhe Hussein Nassoro Amari
Kasu alisema kuwa Katika Wilaya hivyo serikali bado inapoteza kwa kiasi
kikubwa kwa sababu ya kutowarasimisha na kuwapa leseni Wachimbaji
wadogo.
Aidha,
aliiomba serikali kuwapatia leseni Wachimbaji wadogo kupitia vikundi
vyao walivyovianzisha ili kurahisisha ukusanyaji Wa mapato sambamba na
mafanikio ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake.