Waziri wa habari, utamaduni,sanaa na michezo Dokta Harrison
Mwakyembe amewataka wajasiliamali wa vinyago kutafuta zaidi soko la
bidhaa zao za asili ili kukuza kipato na kuendelea kutangaza utalii wa
utamaduni.
Ameyasema hayo alipokuwa akuzunguza na wajasilimali wautalii wa
utamaduni katika soko la Masai,jiji Arusha.Amesema bidhaa za utalii wa
utamaduni ni nembo tosha yakutangaza nchi yetu.
“Ni kweli kuna Changamoto katika ujasiliamali huu wa utalii wa
utamaduni hususani kwenye tozo mbalimbali mnazotozwa na mamlaka husua.”
Serikali ipo tayari kwenye mchakato wakutatua Changamoto hii ya tozo
na kuona ni namna gani soko la vinyago nchini Tanzania linakuwa na
kujulikana zaidi kimataifa, kuliko kwa sasa soko kuu linajulikana lipo
jijini Nairobi wakati wazalishaji wakubwa ni watanzania.
Dokta Mwakyembe alikuwa kwenye ziara ya siku 3 Mkoani Arusha,ambapo
ameweza kufungua redio mpya ya kijamii (TBC FM),aliweza kutembelea kituo
cha redio cha Sunrise,alifungua mkutano wa maafisa habari na mawasilino
serikali,ameweza kukutana na wadau wa utamaduni,sanaa na michezo na
ameweza kutembelea soko la vinyago la jijini Arusha.