SIKU YA WANAWAKE YAADHIMISHWA KWENYE HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo mwakilishi wa Katibu tawala Wilaya ya Arumeru ambaye ndiye mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Magdalena O. John ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha sheria kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru amesema wanawake ni chachu ya maendeleo hivyo ni muhimu kutumia fusra za mikopo wanayopewa kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli za kiuchumi zitakazo inuwa vipato vyao na kushiriki uchumi wa viwanda.
Aidha mwanasheria Magdalena amesema Serikali katiaka kutekeleza kauli mbiu ya siku ya wanawake duniani ambayo ni "Kuelekea uchumi wa viwanda tuimarishe usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake vijijini" Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo( NMB) imeandaa mafunzo mbalimbali kama vile ujasiriamali yatakayotolewa kwa wanawake hao kwa lengo la kuwajengea uwezo wa matumizi sahihi ya mikopo wanayopewa kujikwamu kiuchumi hivyo amewasihi kutumia mafunzo hayo na kuwafundisha wanawake wengine ambao hawajaudhuria mafunzo hayo.
Mwakilishi wa Katibu tawala Wilaya ya Arumeru ambaye ndie mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Magdalena O. John ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha sheria akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
baadhi ya wanawake ambao ni viongozi wa vikundi vilivyonufaika kupewa mkopo na Halmashauri ya Wilaya ya Meru toka kwenye mfuko wa wanawake na vijana wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru .
baadhi ya wanawake ambao ni viongozi wa vikundi vilivyonufaika kupewa mkopo na Halmashauri ya Wilaya ya Meru toka kwenye mfuko wa wanawake na vijana wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru .
baadhi ya wanawake ambao ni viongozi wa vikundi vilivyonufaika kupewa mkopo na Halmashauri ya Wilaya ya Meru toka kwenye mfuko wa wanawake na vijana wakifuatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yanatolewa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru .
baadhi ya wanawake ambao ni viongozi wa vikundi vilivyonufaika kupewa mkopo na Halmashauri ya Wilaya ya Meru toka kwenye mfuko wa wanawake na vijana wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru .
Wanawake ambao ni viongozi wa vikundi vilivyonufaika kupewa mkopo na Halmashauri ya Wilaya ya Meru toka kwenye mfuko wa wanawake na vijana wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru .
Mtoa mada ya ujasiriamali ,Saumu s. Kweka ambaye ni Mratibu wa dawati la uwezeshaji wanachi kiuchumi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza na wanawake kuwa ili wawe wajasiriamali wanatakiwa kuwa wabunifu na kujenga mausiano mazuri na wafanyabiashara wengine .
Hermelinda Kasihwaki ambaye ni Meneja wa Benki ya NMB tawi laUsa-River ameto elimu kwa wanawake juu ya faida ya kutumia benki kuifadhi fedha kuwa ni njia salama na inaepusha matumizi mabaya ya fedha.
Afisa lishe kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru Asia Ijumaa katika utoaji wa mada inayohusu mtindo bora wa maisha amewashauri wanawake kujali afya zao kwa kutumia mlo wenye makundi yote matano ya chakula ambayo yatawapa virutubisho vinavyoitajika mwelini na kuepuka magonjwa yatokanayo na ulaji.
"umuhimu wa kupima ukimwi utakuwezesha kujua afya yako ikiwa hujaathirika utajilinda na kama umeathirika utapewa njia sahihi zitakazo kuwezesha kuishi zaidi na kuepuka maambukuzi mapya "amesema Mratibu wa UKIMWI kwenye Halmashauri ya Meru Grace Mghase wakati wa maadhimisho wa siku ya wanawake kwenye Halmashauri hiyo pia amewasihi wanawake kutokaa kimya bali kuwaelimisha vijana na familia kwa ujumla kujinga na UKIMWI .
mbali na kuwa mwakilishi wa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Meru mwanasheria (wakili) Magdalena O. Johnametoa mada ya wanawake na umilikiwa wa ardhi,sheria ya ndoa na miradhi.