Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara
ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akihutubia wananchi wakati wa mkutano
wa hadhara wa Kijimbo uliofanyika katika Kijiji cha Shibingo Kata ya
Yogelo, Jana 3 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Mbunge
wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko akiwa katika ziara ya Kijimbo kusikiliza kero za
wapiga kura wake, Jana 3 Machi 2018.
Pamoja
na mvua kunyesha lakini baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya
Yogelo Mkoani Geita wakifatilia kwa karibu na umakini mkubwa mkutano
ulioitishwa na Mbunge
wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya Kijimbo kusikiliza kero
za wapiga kura wake, Jana 3 Machi 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwaeleza Baadhi
ya wakazi wa Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo Mkoani Geita
waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara juu ya namna bora ya kuwa na
mafanikio kama Taifa kwa kufanya kazi kwa bidii, Jana 3 Machi 2018.
Na Mathias Canal, Geita
Wanasiasa
hasa wasomi na wale wenye ushawishi mkubwa nchini wametakiwa
kuacha kulalamika na kutoa kauli ambazo hazitawasaidia wananchi katika
kuwatatulia matatizo na kero zao bali waungane na serikali katika juhudi
zinazoonekana za kuleta maendeleo.
Rai
hiyo imetolea na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri
wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa mkutano wa hadhara
na wananchi uliofanyika katika Kijiji cha Shibingo Kata ya Yogelo akiwa
katika ziara ya kijimbo ya siku nne.
Mhe
Biteko amesema baadhi ya wanasiasa maarufu wamekuwa wakitumia muda
mwingi kueleza matatizo na kero za wananchi bila ya kuonyesha suluhisho
au kusaidia kutatua kero hizo jambo ambalo halimsaidii mwananchi kwa
namna yoyote.
Alisema
kuwa Maendeleo ni majumuisho ya mwendelezo wa shughuli za kujiongezea
kipato, amani ya nafsi na uhuru ambapo Maendeleo yeyote ambayo hayana
mwendelezo wa amani ya nafsi, kipato na uhuru, hayo si maendeleo bali ni
mabadiliko yenye ukomo ambayo kwayo hayaleti amani ya nafsi na uhuru wa
kudumu bali kipato cha muda mfupi na furaha ya muda mfupi na mwisho
wake ni mshangao wenye haiba ya huzuni ambatano na maswali yasiyo na
majibu.
"Maendeleo
ni mchakato mi sidhani kama kuna watu hapa ambao wamekamilisha kila
jambo katika familia zao, ila kila siku mnapanga na mnatekeleza jambo
moja baada ya jingine, sasa watakuja watu hapa watasema watawaletea kila
kitu kijijini kwenu, sasa kwa mtazamo wenu jambo hilo linawezekana
kweli? wananchi wakaitikia HAPANA"
Mhe
Biteko alisisitiza kuwa katika kukuza uchumi wa Taifa na mtu mmoja
mmoja wananchi wanapaswa kutambua kuwa wana jukumu kubwa la kushadihisha
maendeleo hayo kwa kufanya kazi kwa weledi.
Aidha,
Mhe Biteko aliwaeleza wananchi kuwa wanapaswa kufanya mambo mawili kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano na wasaidizi wake wote, Mosi ikiwa ni kuunga
mkono juhudi za utendaji lakini pili ni kumuombea ili atomize matakwa
ya wananchi na kusudio la ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya
mwaka 2015-2020.