MHE BITEKO NA MHE MAVUNDE WATINGA MKOANI SHINYANGA KWA ZIARA YA KIKAZI

Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde (Kulia) wakifatilia taarifa ya Mkoa wa Shinyanga mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi,
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Bi Haula Kachwamba akizungumza jambo mara baada ya Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kulia) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde (Kushoto) kuzuru katika ofisi za chama wakiwa katika ziara ya kikazi,
Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo mara baada ya kuwasili Mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi akiwa sambamba na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde

Na Mathias Canal, Shinyanga

Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde leo 27 Februari 2018 wametinga Mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo pamoja na mambo mengine watatembelea mgodi wa EL-Hillal Minerals Ltd.

Mhe Biteko ametinga Mkoani Shinyanga akitokea ziarani Mkoani Tabora huku Mhe Mavunde akiwa ametokea Mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi mwaka 2015-2020.

Wakati Mhe Mavunde akiwa kwenye ziara ya kukagua Viwango vya Kazi na Usajili wa waajiri kwa mfuko wa fidia wa wafanyakazi (WCF) ni sehemu ya kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa agizo la Mhe Jennister Mhagama ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira ambaye aliwataka waajiri wote nchini wawe wamejisajili kwenye mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2017.

Amesisitiza waajiri kujisajili na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kwani kutofanya hivyo Kwa mujibu wa Kifungu cha 71(4) atashitakiwa Mahakamani na akikutwa na hatia adhabu yake ni faini isiyozidi TSh 50,000,000 au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesisitiza umuhimu wa wachimbaji wadogo nchini kulipa kodi huku akieleza kuwa wachimbaji wanapaswa kujiunga kwenye vikundi kwani serikali imetenga maeneo mengine ambayo itatoa wataalamu kuyafanyia Utafiti ili kuimarisha uchimbaji nchini kwa wachimbaji wadogo kuwa wenye tija na hatimaye kuwafanya kutoka katika uchimbaji mdogo kufikia wa kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa.

Pia ameendelea kusisitiza juu ya Wamilili wa Leseni za Madini kote nchini, kutunza takwimu za gharama za uendeshaji wa shughuli zao za uchimbaji na kila Mwezi ziwasilishwe kwa Afisa Madini kwani kutokufanya hivyo wataingia katika mikono ya sheria kwa kulipa faini ya shilingi milioni 50 mpaka milioni 150 au kifungo cha mwaka mmoja jela.

Pia, Mhe Biteko ameeleza dhamira ya ziara yake kuwa anapokuwa katika maeneo mbalimbali anawakumbusha wachimbaji nchini kufuata sheria na taratibu za nchi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post