Shirika la World vision na Tasisi zingine kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Longido wamezindua kampeni kabambe ya kupambana na ukatili wa aina mbalinabali haswa ukatili wa ndoa za utotoni.
Kampeni hizo zimezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo.
Akizindua kampeni hizo ameziasa jamii la Wamasai kumthamini mtoto wa Kike kwa kumsomesha apate Elimu kama Mtoto mwingine.
Amewaambia kuwa kumpa fursa mwanamke ni kulisadia Taifa kutokana na nafasi ya mwanamke katika jamii.
Mh. Chongolo amesisitiza kuwa jambo la ndoa za utotoni halikubaliki kabisa katika jamii yetu.
Alisema kuwa hatakuwa na mzaha katika jambo hili kwani nikumtesa mwanamke katika Maisha yake yote na pia kufedhehesha raifa.
Naye mratibu wa mradi wa mama na mtoto Josia Mluvi aeleza kukidhiri kwa Vitendo vya kikatili kwa watoto ikiwemo ukeketaji na ndoa za utotoni akitaja kazia na simanzi ya msichana aliyekeketwa Mara tatu na kupata maumivu makali yaliyo sababisha kifo wakati wakujifungua.
Alileza mikakati walio nayo yakumkomboa mtoto wa kike wa jamii ya kimasai ambayo ni pamoja na kutunga sheria ndogo za Halmashauri kumlinda mtoto wa kike.
Naye mratibu wa WV alieza lengo la kampeni kuwa ni kumlinda mtoto wa kimasai na vitendo vya ukatili wa ndoa za utotoni na kumuwezesha kupata fursa na elimu itakayoondoa mianya ya ukatili huu.
Naye afisa ustawi wa Wilaya Bi Atuganike aliongeza kuwa katika jamii zetu ukatili umeongezeka sana ambapo kwa mwezi Februari kesi za ukatili wa wasichana zimefika 10 na kati ya hizo 2 zimepelekwa mahakama changsmoto kubwa ikiwa ni kukosekana ushirikiano na ushahidi kwani jamii imekuwa ikiwaficha wahalifu.
Muwakilishi wa Mkuu wa Polisi aliekeza namna ambavyo jamii inamkandamiza mtoto wa kike kwa vitendo vya ukatili. Kesi nyingi zimelundikana na jamii inawakinda wahalifu kwakuwa wanakubaliana kimila nakuwalinda wahalifu.
Mambo mengi yamezungumzwa na mikakati mbalimbali imetolewa. Hivyo ni jukumu la kila mmoja kumlinda mtoto wa kike.