Halmashauri ya Jiji la Arusha imekuwa ikipokea wageni kutoka
miji mbali mbali ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza mambo
mbalimbali ya kiutendaji .
Mnamo Tarehe 16/10/2017 Halmashuuri ya Jiji la Arusha ilipokea wageni
(Naibu Meya, Mkurugenzi, Madiwani na baadhi ya Watendaji) kutoka
Manispaa ya Bukoba ambapo lengo kuu la ziara yao lilikuwa ni kujifunza
juu ya mfumo wa usimamizi wa ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa uzoaji
taka na utekelezaji wa miradi ya uboreshaji miji na majiji
inayofadhiliwa na benki ya dunia (ULGSP na TSCP).
Pamoja na ziraya yao ya kimafunzo pia walipata fursa ya kutembelea
eneo la machinjio ya kisasa yanayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la
Arusha (Arusha Meat) na kujionea namna yanavyofanya kazi kwa usafi na ufanisi wa hali ya juu.
Pia walipata fursa ya kutembelea bustani inayoishi ya Themi (Themi Living Garden)
ambayo katika historia hapo mwanzo ilikuwa kichaka cha wahalifu ila
baadae Halmashuri ya Jiji la Arusha iliamua kuhifadhi eneo hilo na kuwa
mahala pa mapumziko. Kwa sasa linasimamiwa na kampuni ya watu wa Itali,
Oikos baada ya kuingia nao mkataba wa maridhiano juu ya utunzaji wa
mazingira.
Aidha Halmashauri ya Jiji la Arusha Tarehe 19/12/2017 pia ilipokea
Madiwani 42, Wakuu wa Idara 9 na Wataalam watano kutoka Manispaa ya
Morogoro kujifunza Uthamini wa Mali za Halmashauri.