Waendesha bodaboda mkoani Arusha wapewa miezi mitatu kuhakikisha
wanajifunza sheria na taratibu za barabara bila kusumbuliwa na polisi wa
barabarani.
Akitoa kauli hiyo,Waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa Mwigulu Nchemba
katika kikao chake na waendesha bodaboda wa mkoa wa Arusha alipokuwa
akiwagawia kadi za umili wa bodaboda kwa madereva 107 waliofanikiwa
kumaliza mkopo wa mradi wakukopesha pikipiki ulioanzishwa na Mkuu wa
Mkoa wa Arusha.
Kauli hiyo imetolewa na mheshimiwa waziri baada ya Mkuu wa Mkoa wa
Arusha kutoa ombi maalum kwake lakuwaruhusu madereva bodaboda hao
kujifunza sheria kwanza kisha ndio polisi waanze utaratibu wakuwakamata
wale wote watakaokuwa wamekiuka sheria za barabarani.
Mwigulu Nchemba amewasihi bodaboda wote nchini kuchukulia hii kazi
kama yenye heshima ili iweze kuwabadilisha maisha yao na tegemeze wao.
Aidha,amesisitiza utoaji wa leseni kwa bodaboda utazingatia kwa wale
ambao watakuwa wanamiliki kofia mbele na hata akiwa na cheti pia
atapatiwa leseni,pia abiria atakaekaidi kuvaa kofia basi atapatiwa
adhabu yeye nasio dereva kama ilivyokuwa awali.
Akichangia zaidi juu ya mradi huu,Mwiguli Nchemba atachangia kiasi
cha shilingi milioni 10 ilikusaidia vijana wengine waweze kukopeshwa
pikipiki kwa wingi.
Pia, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,amewaambia bodaboda kuwa
wanaweza kutumika katika kubeba watalii ikiwa tu wataweza kufuata sheria
na taratibu za barabarani.
Amewapongeza watendaji kata na maafisa tarafa wa Jiji la Arusha
kwakuonyesha ushirkiano mkubwa katika kufanikisha makusanyo na kwa
wakati, na kiasi cha shilingi milioni 306 tayari zimesharudishwa na
milioni 200 zitatumika kukopesha wamama wajasiriamali wadogo kwa mkopo
wa shilingi laki 2 kwa wamama 500.
Amesema kiasi cha pesa kinachobaki cha zaidi ya milioni 100
kitatumika kukopesha waendesha bodaboda wengine,hii itasaidia
kuwawezesha vijana wengi kumuliki pikipiki zao wenyewe badala
yakutegemea pikipiki za watu wengine ambazo zinawabana sana.
Kamanda wa polisi kitengo cha barabarani Joseph Buberwa,amewataka
bodaboda kuhakikisha wanatii sheria bila shuruti,wapunguze spidi
barabarani hususani kwenye makazi ya watu.
Amesema kuwa polisi barabarani hawatawakamata bodaboda ambao hawana
leseni lakini wana cheti cha udereva na watawapa mda wakuhakikisha
wanapata lesenina amewapongeza madereva 250 waliofanikiwa kuhitimu
mafunzo ya udereva.
Akisisitiza zaidi mwenyekiti waumoja wa madereva bodaboda (UBOJA)
bwana Mauridi Makongoro,amesema mradi huo umewanufaisha sana bodaboda
wengi kwani umewatoa katika mazingira yakuendesha bodaboda za watu
wengine na sasa wanamiliki zao wenyewe na wameweza kuingiza kipato
chakutosha.
Mradi huu ulianzishwa mwaka 2017 na mheshimiwa Gambo kwa lengo
lakuwakwamua bodaboda wa Jiji la Arusha katika changamoto yakukosa mtaji
wakumiliki pikipiki zao, vijana 200 walifanikiwa kukopeshwa pikipiki
hizo na kati yao 107 wamemaliza mkopo nakukabidhiwakadi za umiliki wa
pikipiki na wengine wanaendelea na marejesho.