Ticker

6/recent/ticker-posts

DIAMOND PLATNUMZ NA VANESSA MDEE WAANDIKA HISTORIA MPYA

 
All Africa Music Awards (Afrima) 
 
Huenda yakawa ni mafanikio ya kufungia mwaka katika sekta ya burudani, baada ya Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Vanessa Mdee ‘Vee Money’, usiku wa kuamkia jana kutunukiwa tuzo zilizowataja kuwa ni wasanii bora Afrika Mashariki.
Diamond na Vee Money walishinda tuzo hizo za kimataifa za All Africa Music Awards (Afrima) zilizotolewa usiku wa Desemba 27, huko Lagos, Nigeria.
Vanessa alishinda katika kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki, na kuwashinda Wahu (Kenya), Muthoni The Drmmer (Kenya), Size 8 (Kenya), Kaz (Kenya) na Jackie Chandiru (Uganda).
Diamond Platnumz alinyakua tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki, ambayo alikuwa akiiwania sambamba na Jose Chameleone (Uganda), Kidumu (Burundi), Maurice Kirya (Uganda) na Peter Msechu ft Amini (Tanzania).
Msechu alikuwa akiwania tuzo hiyo kupitia wimbo wake ‘Nyota’ aliomshirikisha Amini.

 13264_1064698616877889_8527567974793583869_n
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Msechu alionekana akiwa amebeba tuzo ya Diamond ambaye hakuhudhuria katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo, kutokana na ziara yake ya kimuziki huko Bujumbura, Burundi ambako alifanya shoo usiku wa kuamkia leo.
Vee Money ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha redio cha Choice FM na MTV Base, kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliandika “kwa Mungu kuna utukufu, asanteni sana kwa kunipigia kura. Ninawapenda ‘Best Female EastAfrica Tanzania.”
Wanamuziki wengine kutoka Afrika Mashariki waliopata tuzo hizo ni pamoja na Elani kutoka Kenya aliyetajwa mshindi wa tuzo ya Wimbo Bora wa Pop, huku Radio na Weasel kutoka Uganda, wakipata tuzo ya Wimbo Bora wa Reggae.
Nigeria waingiwa hofu
Ushindi huo wa kishindo kutoka Tanzania, umewafedhehesha wanamuziki mbalimbali kutoka Afrika Magharibi, Kusini na Afrika Mashariki ambao wameonyesha wazi kuanza kuifikiria Tanzania katika mapinduzi ya muziki kwa mwaka 2015.
Mwanamuziki Davido ameendeleza hofu yake kwa wasanii wenzake, baada ya kushindwa kumuunga mkono msanii mwenza na rafiki yake Diamond Platnumz, mara baada ya kutajwa kuwa mshindi wa tuzo usiku huo.
Tanzania imeanza kung’ara kimuziki dhidi ya mataifa mengine, huku wanamuziki wake wakiwaburuza wenzao wa Afrika Mashariki.

Post a Comment

0 Comments