Sakata hilo limetokea leo majira ya saa 4:00
asubuhi, muda mfupi baada ya Wakili wa Serikali, Peter Njike kumueleza
Hakimu Mkazi, Hellen Liwa kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa,
upelelezi wake bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine
kwa kutajwa.
Sakata hilo limetokea leo majira ya saa 4:00
asubuhi, muda mfupi baada ya Wakili wa Serikali, Peter Njike kumueleza
Hakimu Mkazi, Hellen Liwa kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa,
upelelezi wake bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine
kwa kutajwa.
Baada ya wakili Njike kueleza hayo, mshtakiwa
Longishu Losingo alidai mahakamani hapo kuwa Desemba 16,2014 upande wa
mashtaka uliwaambia jalada la kesi yao lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka
(DPP), leo (jana) wanatuletea hadithi, tunaomba watueleze uhalisia wa
kesi hii, tupo gerezani tunateseka.
Kwa upande wa mshtakiwa Masunga Makenza naye
alidai kuwa yeye hafahamu sheria, kesi yao ni ya muda mrefu na akahoji
jalada likienda kwa DPP linatakiwa kukaa kwa muda gani.
Makenza alidai kuwa kesi yao ni ya kubambikiwa na
kwamba ingekuwa ni kesi halisi upande wa mashtaka ungekuwa umekwisha
kamilisha upelelezi wao na kwamba wao wapo tayari kushtakiwa ila kama
upande wa mashtaka umeshindwa kukamilisha upelelezi mahakama iwaachie
huru, wakikamilisha watawakamata tena.
Wakili wa Serikali, aliieleza mahakama kuwa
wameyasikia malalamiko hayo na kwamba yote yanajikita katika kuchelewa
kukamilika kwa upelelezi na kwamba watahimiza na kufuatilia upelelezi
ukamilike mapema.
Jibu hilo halikuwaridhisha washtakiwa hao,
mshtakiwa Longishu alisema “Tumechoka kwa kweli tumechoka hatuna ugomvi
na mahakama wala magereza ila tunaugomvi na waendesha mashtaka kama
wameshindwa kukamilisha upelelezi watupeleke polisi.”
Yote kwa yote washtakiwa hao, wakaiambia mahakama
kuwa kutokana na hoja hizo za upande wa mashtaka leo (jana) hawapo
tayari kushuka kizimbani, watakaa chini hadi waelezwe jalada leo lipo
wapi na kesi imefikia katika hatua gani.
Baada ya washtakiwa hao wote kugoma kushuka
kizimbani na kukaa chini wakisubiri kuelezwa hatma ya kesi yao, Hakimu
Liwa aliwasihi wakubali kuondoka kizimbani hapo kwa sababu yeye siyo
hakimu husika ameitaja tu kesi yao, wamsubiri hakimu husika, Waliarwande
Lema wamueleze malalamiko yao.
Maelezo hayo ya hakimu Liwa walikubaliana nayo na
kwa pamoja wakainuka na kuelekea mahabusu ya mahakama kwa ajili ya
kupelekwa mahabusu na kesi iliahirisha hadi Januari 13,2015.
Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni
Chibago Magozi (32), John Mayunga (56),Juma Kangungu (29), Paulo
Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40), Zacharia Msese (33), Msungwa Matonya
(30), Ahmad Kitabu (30).
Kwa pamoja wanadaiwa kuwa Novemba 3, mwaka
2013, walifanya kosa hilo la mauaji kinyume na kifungu cha 196 cha
sheria na kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka
2002.
CHANZO;mwananchi
CHANZO;mwananchi