Diwani
wa Viti Maalum Ngorongoro Tina Timan akizungumza wakati wa mkutano na
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alitaka mamlaka
husika kubadili sheria kandamizi ili jamii ya Wamasai wafaidike na ardhi
yao .
Mwakilishi
wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Diwani Viti Maalum Maanda Mgoitiko
akichangia mada wakati wa mkutano wa Wawakilishi wa Mabaraza ya Wazee
wa Kimila wa Kimasai na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Mzee wa Kimila kutoka Ngorongoro Jerubi Mkati akizungumza wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Lembulung
Ole Kosyando kutoka Kiteto akizungumza juu ya migogoro ya ardhi
inayowakabili ambapo alisema viongozi wa kiserikali na wa kisiasa
wanamiliki ardhi kubwa kinyume na taratibu kiasi cha kuleta migongano
mikubwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza kwa makini pamoja na Mbunge wa Longido Ndugu Michael Lekule Laizer (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Onesmo Ole Nangole.
Sarah
Yohana akizungumzia namna wanawake wa Kiteto wanavyoishi kwa mashaka
kutokana na maisha yao kuwa hatarini na kuitaka serikali kufanya juhudi
katika kutatua migogoro iliyokithiri Kiteto.
Doroh
M. Kipuyo Diwani wa Monduli (Wanawake) akizungumzia jinsi wamasai
wanavyoumia kuona Serikali haichukui hatua za haraka kwenye matatizo
yanayowakabili.
Wazee
wa Kimila wa Kimasai wakiandika yale muhimu wakati wa mkutano na Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika Namanga.
Leboi
Sumuni kutoka Monduli akielezea namna wamasai walivyo na mapenzi na
Chama Cha Mapinduzi na kutaka Chama hicho kionyeshe mapenzi kwa wamasai
kwa kusaidia kutatua kero zao ambazo zinaonekana kuwa kubwa siku hadi
siku.
Wazee wa Kimila wakifuatilia mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana( kulia) akisikiliza kwa makini wazee wa kimila wa Kimasai pamoja na Mbunge wa jimbo la Longido Michael Lekule Laizer ambaye alisaidia kutafsiri baadhi ya hoja zilizozungumzwa kwa lugha ya kimasai.
Philipo
Kiloe Laiser Diwani wa kata ya Lubomba Longido akizungumzia Wazee wa
Kimasai na kuwaelezea kuwa ni watu wenye hekima busara na wanatambulika
kwenye jamii.
Esupat
Ngulupa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido akichangia jambo
wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mzee wa Kimila wa Kimasai wakifuatilia kwa makini mkutano huo ambao ni hatua zaidi za kutafuta suluhisho la migogoro yao .
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Onesmo Ole Nangole. akiongea machache kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu kuongea.
Mbunge wa Longido Michael
Lekule Laizer akizungumzia masuala mbali mbali yanayoikabili wamasai
na namna ya kuyatatu ikiwa pamoja na kujengwa kwa viwanda
vitakavyodhalisha bidhaa zitokanazo na mifugo.
Mbunge wa Kiteto Benedicto Ole Nangole akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mbunge
wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka akichangia mada wakati wa
mkutano wa Wazee wa Kimila wa Kimasai na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana ambapo alisema suala zima la ajira liwe kwenye uwiano
wa sura ya nchi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wazee wa Kimila wa
Kimasai na kuahidi kuyafanyia kazi matatizo yanayowakabili kwa muda
mrefu kwa kushirikiana na wabunge wa CCM
Viongozi wakimila wakimsalimia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe la baraza la Wazee wa Kimila mara baada ya kumaliza mkutano.
Tags
MATUKIO HABARI