MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kutuhumiwa na tukio la kumteka mtendaji wa
kata ya makiba .
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa
wa Arusha Lebaratus Sabas alisema kuwa mtuhumiwa huyu alikamatwa majira ya saa
moja usiku December 16 katika eneo la
Doli lililopo katika kijiji cha Usa -river
kwenye gari aina ya land Gruzer lenye namba za usajili T 753 AQR.
Alisema kuwa mbunge
huyo anatuhumiwa kumteka mtendaji kata aliyefahamika kwa jina la Nemani
Ndundu wa kata ya makiba tarafa ya
Mbuguni wilayani Arumeru mkoani Arusha December
15 majira ya saa mbili asubui katika
eneo la maji ya chai .
Alibainisha kuwa mtendaji huyo alikumbwa na tukio hilo
wakati alipokuwakatika pikipiki yake akielekea kwenye kata yake ndipo mbunge
huyo alimkamata na kumpiga na kumjeruhi katika sehemu mbalimbali za mwili wake
huku akimtaka amuonyeshe majina ya wanachama waliopiga kura katika kituo cha huduma na maendeleo kilichopo katika kata yake
.
Aidha kamanda sabas alisema kuwa mpaka sasa Joshua Nassari anashikiliwa na
polisi na anatarajiwa kufikisha mahakamani
ya wilaya ya Arumeru leo December 17 kujibu tuhuma zinazomkabili.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia