Meneja
wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa
bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village huku akipewa
sapoti na Digna Mbepera.
Digna
Mbepera na Bela Kombo wakimpa back up Aneth Kushaba AK47 kwenye show
zao za kila Ijumaa ndani ya viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
Majembe ya Skylight Band yakionyesha manjonjo yao jukwaani Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki.
Aneth Kushaba na Sam Mapenzi wakiwapa raha mashabiki wao huku Digna Mbepera na Bella Kombo.
Sam Mapenzi na Aneth Kushaba AK47 wakifanya yao jukwaani.
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakiserebuka mdogo mdogo.
Birthday girl nae hakubaki nyuma aliunga tela na kuburudika na Skylight Band.
Msanii
wa bongo movie Kajala akitembeza manoti ya wekundu wa msimbazi kwa
waimbaji wa Skylight Band Ijumaa iliyopita alipokunwa na uimbaji wao.
Kajala akizichomoa tu kwenye pochi lake.
Joniko Flower akisubiria zamu yake.
Joniko Flower akipokea manoti yake kutoka kwa Msanii wa bongo movie Kajala.
Na kwa wale wasanii waliokuwa back stage pia walibahatika kujizolea manoti kutoka kwa Kajala.
Wapenzi wa Skylight Band wakishuhudia tukio hilo.
Twende kazi... na burudani iendeleeee..!
Mashabiki nao wakajibu mapigo.
Sam Mapenzi akitunzwa na shabiki wake.
Sam Mapenzi akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band, Ijumaa iliyopita huku Joniko Flower na Sony Masamba wakimpa sapoti.
Mashabiki wakiendelea kula raha..!
Birthday girl na mabeste zake wakicheza mdogo mdogo.
Mguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma...... mashabiki wakiondoka ma-style ya Skylight Band.
Hashim
Donode na Bela Kombo wakiburudisha mashabiki wa Skylight Band huku
wakipewa back up na Aneth Kushaba pamoja na Digna Mbepera.
nakupenda
pia pia aha...Nakupenda pia...You make me wanna say....Nakupenda pia
pia ahaa.....Vijana wakiwa kwenye hisia kali jukwaani.
Majembe ya Skylight Band yakisebeneka jukwaani huku yakijaribu kuwafundisha mashabiki wao.
Mkongwe
wa muziki wa dansi nchini, Joniko Flower akiwachezesha ligwaride la
sebene majembe ya Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village .