BREAKING NEWS

Monday, December 15, 2014

HAYA NDIO MATOKEO YA AWALI YA UCHAGUZI SEREKALI ZA MITAA


Kilimanjaro
Katika Kitongoji cha Njiapanda Magharibi (Vunjo) CCM ilishinda kwa kura (343), NCCR-Mageuzi (195) na TLP-(36).
Katika Kitongoji cha Njiapanda Mashariki (Vunjo), NCCR-Mageuzi imeshinda kwa kura (277), CCM (239), Chadema (71) na TLP (37). Katika Kitongoji cha Faru (Vunjo) Chadema imeshinda kwa kura (288), CCM (93), TLP (27) na NCCR-Mageuzi (7). Katika Kitongoji cha Darajani (Vunjo), NCCR-Mageuzi imeshinda (208), CCM (204), Chadema(169) na TLP (46). Kitongoji cha Kashinda (Vunjo), NCCR-Mageuzi imeshinda kwa kura 31, CCM (19) na Chadema (13). Kitongoji cha Makere NCCR-Mageuzi imeshinda kwa kura 52, CCM (20). Kitongoji cha Ofisini Chadema imeshinda kwa kura 43, NCCR-Mageuzi (20) na CCM (12).
Katika Kijiji cha Marawe Kirua (Vunjo), CCM imeshinda kwa kura 164, Chadema (77), NCCR-Mageuzi (84) na TLP (43). Katika Manispaa ya Moshi Mtaa wa Rengua, Chadema imeshinda kwa kura 83 na CCM (58). Mtaa wa Bonitte, Chadema imeshinda kwa kura 65 na CCM (51). Mtaa wa Kiusa CCM imeshinda kwa kura 143 na Chadema (95). Mtaa wa Korongoni Chadema imeshinda kwa kura 252 na CCM (244). Mtaa wa Sabasaba CCM imeshinda kwa kura 228, Chadema (114) na katika Mtaa wa Kambaita CCM ilishinda kwa kura 172 na Chadema(171).
Kilindi
CCM imepita bila kupingwa katika vitongoji 615 na vijiji 102. Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Kilindi, Daudi Maige alisema jana kuwa kutokana na CCM kupita bila kupingwa katika vijiji 102 na vitongoji 615 uchaguzi ulilazimika kufanyika katika vijiji viwili tu, Kileguru na Makasini.
Mbeya
Mtaa wa Sabasaba nafasi ya Mwenyekiti CCM, Aidan Ng’oma, kura 74 wakati Anna Mwenda wa Chadema akipata kura 23. Mtaa wa Kisoki mgombea wa uenyekiti Edward Mwakasiti wa CCM alitangazwa mshindi baada ya kupita bila kupingwa.
Katika Mtaa wa Mwasyoke, uchaguzi wa mwenyekiti uliahirishwa, lakini kwa upande wa wajumbe, CCM ilipata viti vitatu wakati Chadema ilipata viwili. Mtaa wa Itezi, mgombea wa CCM, Anania Sanga alipita bila kupingwa, kama ilivyokuwa kwa Daud Kipenya wa chama hicho kwa Mtaa wa RRM.
Kutoka Vwawa mgombea wa uenyekiti Kitongoji cha Masaki (Chadema) alipata kura 96 wakati CCM ilipata kura 48.
Arusha
Chadema kimeendelea kukitesa CCM wilayani Karatu, baada ya kushinda viti 24 kati ya 27 katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Karatu. Katika Mtaa wa Mazingira Bora, Chadema ilishinda kwa kura 260, CCM kura 137. Kitongoji cha Bomani, Chadema ilishinda kwa kura 251 na CCM ilipata kura 177. Karatu Kati, Chadema kura 281, CCM, 109.
Kigoma
Katika Kata ya Mwandiga, Kigoma katika matokeo ya awali hadi tunakwenda mitamboni CCM ilikuwa imeshinda mitaa minane, ACT minane na ADC mtaa mmoja.
Dar es Salaam
Katika Mkoa wa Dar es Salaam, matokeo yalichelewa kutangazwa katika baadhi ya maeneo na kusababisha malalamiko kutoka kwa baadhi ya wapigakura waliokuwa wakihisi kuwapo kwa uchakachuaji.
Katika Mtaa wa Kwa Mzungu, Kilungule, Temeke, CCM ilishinda kwa kura 378, CUF 303 na zilizoharibika ni 185.
Katika Mtaa wa Kivukoni, CCM kimeshinda kwa kura 183, Chadema (65). Mtaa wa See View, CCM imepita bila kupingwa. Matokeo hayo yametangazwa na msimamizi msaidizi Renatus Luhungu.
Mtaa wa Segerea Migombani, Chadema imeshinda kwa kura (547), CCM (273), NCCR-Mageuzi (205). Mtaa wa Hananasif Kinondoni, CCM imeshinda kwa kura 472, Chadema (231).
Dodoma
Katika Manispaa ya Dodoma CCM, imeshinda katika Mtaa wa Msangalaleli Magharibi kwa kura 110 huku Chadema ikipata kura 38. Katika Mtaa wa Msangalaleli Mashariki, CCM ilishinda kwa kura 180 na Chadema 26. Mtaa wa Nzuguni A, CCM imeshinda kwa kura 408 na Chadema kupata kura 67. Mtaa wa Chang’ombe Juu, CCM imeshinda kwa kura 325, Chadema (120). Mtaa wa Bwawani, CCM 110, Chadema (40).
Iringa
Katika Mtaa wa Migombani, CCM imeshinda kwa kura 70, Chadema 58. Mtaa wa Frelimo A, CCM imeshinda kwa kura 123, Chadema 83. Mtaa wa Kondoa, Chadema imeshinda kwa kura 113 na CCM 109. Mtaa wa Darajani Chadema imeshinda kwa kura 109 na CCM (86). Katika Mtaa wa Kihesa Sokoni, Chadema imeshinda. Mtaa wa Ngeleli, CCM imeshinda kwa kura 115, Chadema (94). Mtaa wa Kidunda Chadema imeshinda kwa kura 73, CCM (69).
Katika Kijiji cha Nyabula, Wilaya ya Iringa, Chadema imeshinda kwa kura 110, CCM (72).
Morogoro
Hadi tunakwenda mitamboni CCM ilikuwa imeshinda katika mitaa 18. Katika mitaa mitano miongoni mwa hiyo sita, wagombea wa CCM wamepita bila kupingwa na katika mtaa mmoja, mgombea wa chama hicho, amemshinda mgombea wa CUF.
Katika Kata ya Mbuyuni, CCM imeshinda kura 149, CUF (63). Kata ya Mwembesongo CCM imepata ushindi katika mitaa minane kati ya 16.
Mwanza
Mamlaka ya Mji Mdogo Nansio, Ukerewe, CCM imeshinda viti vitano huku Chadema na CUF wakiambulia kiti kimojakimoja.
Katika Mamlaka ya Mji wa Sengerema wenye mitaa 11 yote imechukuliwa na Chadema.
Mirerani
Katika Kata ya Mirerani Chadema imeshinda Vitongoji 7 kati ya 8.
Bunda
Hadi tunakwenda mtamboni katika, vitongoji 15 vya mjini Bunda na Nyamuswa CCM ilikuwa imeshinda Vitongoji saba, Chadema saba na CUF kimoja.
Njombe
Mtaa wa Posta, Chadema imeshinda kwa kura 218, CCM (216). Mtaa wa Joshoni, CCM imeshinda kwa kura 210, Chadema (155). Mtaa wa Kambarage, Chadema imeshinda kwa kura 479, CCM (288).
Imeandikwa na Burhani Yakub, Joseph Lyimo, Daniel Mjema, Hawa Mathias, Stephano Simbeye, Mussa Juma na Hakimu Mwafongo na Geofrey Nyang’oro, Sharon Sauwa, Shaban Lupimo, Jovither Kaijage, Salum Maige na Christopher Maregesi.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates