Kampuni ya Tanzanite
One iliyopo Mererani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara imeuza hisa zake zote kwa
kampuni ya Sky Associates Group inayomilikiwa
na watanzania.
Tanzanite
One ambayo ni kampuni tanzu ya Richland Resource ya nchini Uingereza inayongozwa
na Mkurugenzi Mtendaji Bernard Oliver imeamua kuu hisa zake asilimia 50 kwa
wazawa hao kutokana na kampuni ya Tanzanite One kukumbwa na madeni na kushindwa
kujiendesha na kukabiliwa na deni la shilingi bilioni 23.
Wakurugenzi wa
kampuni ya Sky Associates Group ,Hussein Gonga na
Faisal Shahbhati wamethibitisha kununua hisa zote za Tanzanite One baada ya
kampuni hiyo kujitangaza katika mitandao yake ya kibiashara kuwa imeshindwa kujiendesha
kutokana na migogoro kati ya kampuni hiyo na wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakivamia migodi hiyo mara kwa
mara na hakuna ulinzi madhubuti.
Mkurugenzi
mwingine aliyemo katika kampuni ya Sky Associates iliyonunua hisa za Tanzanite
One Rizwan Ullah raia wa india ambaye ana hisa kidogo tu katika kampuni hiyo.
Kwa mujibu
wa uchunguzi uliofanywa na gazeti na kuona baadhi ya nyaraka Sky Associates
Group imenunua hisa za tanzanite One na
mali za kampuni hiyo kwa thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 32 fedha za
kitanzania.
Uchunguzi
umebaini kuwa Sky Associates Group imechalipa bilioni 27 ikiwa ni pamoja na madeni
na kumiliki mali za kampuni ya Tanzanite One na bado inadaiwa dola za
kimarekani milioni 5.1 sawa na fedha za kitanzania shilingi bilioni 8.9
Habari za
ndani ya kampuni ya Tanzanite One zinasema kuwa madeni makubwa yanayoikabili
kampuni hiyo ni pamoja na taasisi za serikali na wabia wengine wa kampunbi hiyo
na kufikia kiwango hicho cha shilingi bilioni 23.
Uchunguzi
umebaini pia kuwa kampuni ya Sky Associates Group mbali ya kumilikiwa na wazawa
kwa asilimia mia moja lakini imesajiliwa nchini Hong kong na wakurugenzi wa
kampuni hiyo wamekuwa wakifanya biashara ya madini katika nchi mbalimbali
duniani.
Akizungumzia
kununua hisa za kampuni ya Tanzanite One,mmoja wa wakurugenzi wa Sky
Associates,Hussein Gonga alikiri yeye na mwenzake Faisal kununua hisa za
Tanzanite One na hisa nyingine asilimia mia kumilikiwa na serikali.
Gonga
alisema kwa sasa ninachoweza kusema ni kweli yangu imenunua hisa zote za
Tanzanite One na kuna taratibu nyingine za kisheria zinafuata na taratibu hizo
zikikamilika atatoa taarifa rasmi.
‘’Ni kweli
sisi wazawa tumeigomba Tanzanite One kwa kununua hisa zake baada ya kukabiliwa
na mzigo mkubwa wa madeni na kushindwa kujiendesha kibiashara’’alisema Gonga
Kampuni ya
Sky Associates Group mbali ya kufanya biashara ya madini pia imekuwa ikifanya
utafiti ,kutangaza madini yasiyotambulika lakini yana soko zuri Ulaya na Asia ambayo
yanachimbwa sambamba na Tanzanite .
Miongoni mwa
madini hayo amabyo kampuni hiyo inayatangza ni pamoja na pink tanzanite,yellow
tanzanite,Axinite,Grossular Garnet,Kyenite na Diopsite.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia