Wabunge
wa Kenya wametofautiana pakubwa bungeni kufuatia mjadala kuhusu mswaada
tatanishi wa usalama ambao wabnunge w aupinzani wanasema unakiuka uhuru
wa wakenya.
Bunge
lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili
mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao
maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye
utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.
Mwenyekiti
wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyaja
mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza
kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado
mapambano.'
Spika wa
bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa bunge kuwaondoa
baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa
kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.
Mswada
huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na
mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza
kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.
Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.
Pia ikiwa
mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa faini
ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha ambazo
zinaleta hofu na kusababisha taharuki.
Mswada
huu umetolewa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al
Shabaab wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia
Rais
Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa tangui
mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari
la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.