Hatma ya
mvulana mwenye asili ya China anayeishi na virusi vya ugonjwa wa ukimwi
,imetaarifiwa amelazimika kuhama nyumbani kwao baada ya wanakijiji
wapatao 200 kumtaka kuhama.
Kisa
chake kinatanabahisha kiwango cha unyanyapaa kwa wanaoishi na virusi vya
ukimwi nchini China,pindi wanapotambulika basi hukumbana na unyanyapaa.
Mlezi wa
motto huyo ambaye ni babu yake,alikuwa ni miongoni wanakijiji waishio
kusini magharibi katika jimbo la Sichuan waliosaini makubaliano ya
kumuwinga mvulana huyo mwenye umri wa miaka nane ili kulinda afya ya
wanavijiji hao .
Taarifa
zinaeleza kwamba mvulana huyo aliupata ugonjwa huo kutoka kwa mama yake
mzazi,na aligunduliwa kwa mara ya kwanza kama ana ugonjwa huo mnamo
mwaka 2011, alipokwenda kupata matibabu hospitalini baada ya kuumia.
Unyanyapaa
haukuishia hapo kwa mvulana huyo kwani kila shule aliyokwenda kutaka
kujiunga nayo ilia pate elimu walimkataa, na wanakijiji hawataki hata
kuchangamana naye.
Na Kunkun
kwa jina alilopewa la utani analalama akisema,hawataki hata kucheza
nami,nacheza peke yangu, na wananiona kama bomu linalotaka kulipuka
wakati wowote.
Pamoja na
kumnyanyapaa na kutotaka kuchangamana naye, wanakijiji hao wanadai
wanamuonea huruma,hana hatia na ni motto mdogo, lakini wakadai kuwa
virusi alivyonavyo vinawatisha.
Wanakijiji
hao wanadai mama wa mvulana huyo alifariki mnamo mwaka 2006,wakati baba
wa mvulana huyo hajulikani alipo baada ya kujua afya ya mwanawe na
hivyo kumtelekeza. Elimu kwa jamii ya raia wa China juu ya ugonjwa wa ukimwi ni finyu, na hivyo kusababisha unyanyapaa na hofu miongoni mwao.
Wizara ya
afya ya China na masuala ya uzazi wa mpango imeeleza takwimu
zinazoishia mwezi October mwaka huu zinaonesha kwamba watu walioathiriwa
na virusi vya ugonjwa huo ni laki nne na elfu tisini na saba,nah ii ni
tangu mgonjwa wa kwanza kugunduliwa nchini humo mwaka 1985,na
inakadiriwa kuwa china ina watu bilioni 1.36.
Suala la
unyanyapaa dhidi ya ugonjwa huo ni changamoto inayokabili
shule,hospitali,maeneo ya kazi na kwingineko nchini China,nah ii ndio
sababu ya kudumaza harakati za kutambua na kupamba na virusi hivyo.