Jeshi la polisi mkoa arusha linamshikilia mbunge wa jimbo la Arusha mjini godbless lema kuhusiana na tuhuma za vurugu zilizotokea Aprili 24 katika chuo cha uhasibu njiro kufuatia kuwawa kwa mwanafunzi mwenzao kwa kupigwa kisu na kufariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Arusha kwa vyombo vya habari Lebaratu Sabas amesema kuwa muheshimiwa mbunge alikamatwa Aprili 26 majira ya saa tisa 9:10 usiku nyumbani kwake na kumfikisha katika kituo kikuu cha polisi .
Kamanda Sabas alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea kumuhoji mbunge huyo kuhusiana na vurugu hizo ambapo alibainisha kuwa wakati akihojiwa muheshimiwa lema atakuwa na mwanasheria wake .
Sabas alisema kuwa jeshi la polisi linatarajia kumfikisha muheshimiwa huyo mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili huku watuhumiwa wengine kumi na nne 14 wakiwa wameshafikishwa mahakamani kutokana na vurugu hizo.
Aidha kamanda wa polisi alisema kuwa hakuna nguvu zozote zilizotumika kumkamata muheshimiwa huyo bali kutokana na kutojisalimisha lililaizimu jeshi la polisi kuizingira nyumba yake ndipo alipo jisalimisha mwenyewe.
Kufuatiwa kukamatwa kwa mbunge huyo wa jimbo la Arusha mjini ni kuhusiana na taarifa ya mkuu wa mkoa kupitia kwa vyombo vya habari baada ya vurugu kutokea katika chuo uhasibu njiro na baadhi ya watu kukamatwa akiwemo mwanasheria wake Alibarti Msando likimtaka lema kujisalimisha mwenyewe na kuweza kuisaida polisi kuhusiana na vurugu hizo kwenye kituo chochote cha polisi ambapo muheshimiwa huyo hakufanya hivo huku jeshi la polisi likiwa linamtafuta ambapo ililazimu jeshi hilo kuzingira nyumba yake na hatimaye akajisalimisha mwenyewe.
kuhusiana na taarifa ya kukamatwa kwa mwanasheria wa lema siku ya vurugu kamanda sabas amekanusha na kusema kwamba hakuna mwanasheria aliekamatwa bali mwanasheria aliopo ndani ni maombi ya mbunge lema kuomba mwanasheria wake awepo wakati anaojiwa.
Kwa upande wa mkuu wa mkoa akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa alipokea ujumbe wa manene(sms) ya kumtishia jambo ambapo mkuu wa mkoa amekanusha na kumtaka lema athibitishe kwa kupita kampuni iliyohusika .
Vurugu hizi zilitokea Aprili 24 baada ya kuwawa kwa mwanafunzi Hendry Kogo (22) mwanafunzi wa mwaka wa pili mahesabu na fedha ambaye aliuwawa nje ya chuo maeneo kati ya kanisa la sabato na geti ya chuo majira ya saa nne usiku ambapo bado kifo chake kizungumkuti kwamba alitoka hostel kwenda chuo au chuo kenda hostel.