Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe jana asubuhi katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia Shughuli za uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu waliofariki imeelezwa kuwa imefikia 2o na waliookolewa wakiwa hai ni 17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo la tukio baada ya kuangalia Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe jana asubuhi katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia Shughuli za uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu waliofariki imeelezwa kuwa imefikia watatu na waliookolewa wakiwa hai ni 17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova
Hali ilikuwa hivi
Wasamaria wema wakijaribu kufanya uokoaji
Vijana walikuwa wakicheza mpira jirani na jengo hilo nao walijeruhiwa vibaya
Magari yalifukiwa na kuharibika vibaya
TAARIFA YA UHAKIKIKA KABISA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE
INAELEZA KUWA JENGO MOJA LA GHOROFA 16 LILIPO JIRANI NA MSIKITI WA
SHIA ULIOPITA KATIKA MTAA WA IDRA GHAND,KATIKATI YA JIJI LA DAR ES
SALAAM,LIMEPOROMOKA MUDA MFUPI ULIOPITA
INAELEZWA KUWA MPAKA SASA WATU 17 WAMEOKOLEWA HUKU WAWILI WAKIWA
WAMEPOTEZA MAISHA,NA JUHUDI ZA ZIADA ZINAENDELEA KUFANYWA ILI KUOKOA
WENGINE WENGI WALIOFUKIWA NA KIFUSI HICHO.
MKUU WA MKOA WA JIJI LA DAR ES SALAAM,MH. SAID MECK SADICK
PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE MBALIMBALI WAPO ENEO LA TUKIO HIVI SASA
AKISHIRIKIANA NA WADAU WENGINE WA VYOMBO MBALI MBALI VYA ULINZI NA
USALAMA,KUHAKIKISHA UOKOAJI UNAFANYIKA KWA WAKATI. AIDHA UHABA
WA VIFAA VYA UOKOAJI UNAWEZA KUCHELEWESHA ZOEZI HILO LA UOKOAJI.
MINONGONI MWA VIFAA VINAVYOHITAJIKA HAPO NI PAMOJA NA MASHINE ZA
KUPASULIA ZEGE, SCAVETA KWAAJILI YA UFUKUAJI.
CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA JENGO HILO HAKIJAFAHAMIKA MPAKA SASA,KWANI KILA MTU YUPO KWENYE HEKAHEKA ZA UOKOAJI.
HATA HIVYO HABARI ZA NDANI ZINASEMA WATU 17 WAMEOKOLEWA NA WATU 2 WAMEKUTWA WAMEKUFA ILA BADO ZOEZI LA UHOKOAJI LINAENDELEA
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia