Mh
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha maombolezo alipofika
mkoani Arusha leo Kuwapa pole ndugu na jamaa ambao ndugu zao wamefariki
katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha.
Maporomoko hayo yametokea jana na kusababisha vifo vya watu13 na
majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine amelazwa katika
Hospitali ya Mount Meru
Waziri Mkuu akiwa na wabunge wa Arusha na Meya pamoja na mkuu wa mkoa
kwenye msiba huo mzito. Toka Kushoto ni Mbunge wa Arusha Mjini Mhe
Godbless Lema, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Magessa Mulongo, Meya wa jiji
la Arusha Mstahiki Gaudence Lyimo, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe
Joshua Nassari na Mbunge wa kuteuliwa Catherine Magige
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Peter Pinda
hii leo aliungana na waombolezaji wengine katika misa ya pamoja kuaga
miili ya vijana waliokufa kwa kuangukiwa na gema la mchanga maeneo ya
Moshono jana, Jijini Arusha.
Mh Pinda baada ya kumaliza tukio hilo, yeye na msafara wake muda huu wakaelekea yaliko machimbo hayo yaliyoleta maafa..
Mh Pinda baada ya kumaliza tukio hilo, yeye na msafara wake muda huu wakaelekea yaliko machimbo hayo yaliyoleta maafa..
Sehemu ya majeneza ya marehemu katika ibada hiyo maalumu leo
Waziri Mkuu akipeana mkono na Askari wa Jeshi la Wananchi (jwtz) alipotembelea eneo la tukio.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda alipowasili mkoani Arusha leo Kuwapa pole ndugu na
jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo ya Moramu katika eneo
la Moshono Mkoani Arusha, maporomoko hayo yametokea jana nakusababisha
vifo vya watu 13 na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine
amelazwa katika Hospitali ya Maunti meru.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akitoka eneo la tukio katika machimbo ya Moramu
katika eneo la Moshono Mkoani Arusha, maporomoko hayo yametokea jana
nakusababisha vifo vya watu 13 na majeruhi wawili.
Picha zote na Chris Mfinanga
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia