Ticker

6/recent/ticker-posts

AIBUKA NA KUDAI KUGUNDUA DAWA YA KUTIBU SARATANI

 
 
Mtaalamu wa tiba za asili nchini,Profesa Japhet Laiser amedai kugungua dawa inayotibu maradhi ya saratani kupitia mmea wa asili ujulikanao kama Plumbago Zaylanicum.

Mtaalamu huyo alidai kugundua dawa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha ambapo alidai kuwa tayari dawa hiyo imeshaanza kutibu wagongwa mbalimbali na kuonyesha mafanikio.

Akiongea na waandishi wa habari Prof,Laiser alisema kuwa dawa hiyo inatambulika na kisheria na taasisi ya utafiti ya magonjwa ya binadamu(Nimri).

Hatahivyo,alisisitiza ya kuwa kabla ya kugundua dawa hiyo alifanya utafiti kwa kipindi cha miaka miwili katika kituo cha utafiti cha magonjwa ya binadamu kilichopo eneo la Ngongongare wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Prof,Laiser alisema kuwa wakati akifanya utafiti wa dawa hiyo alikuwa akishirikiana bega kwa bega na jopo la watalamu wa utafiti wa magonjwa ya binadamu hapa nchini.

Hatahivyo,alienda mbali na kudai kuwa tayari ameshaweka utaratibu wa kuiwekea hakimiliki dawa hiyo ili kuepuka kuporwa haki zake katika siku za usoni na watu wajanja.

Aliwataka watanzania kujitokeza kuchangamkia dawa hiyo kwa kuwa tayari imeshaanza kuonyesha mafanikio kwa baadhi ya wagonjwa ambapo kwa sasa alidai anaisambaza katika mikoa mbalimbali nchini.

Hatahivyo,alitoa tahadhari kwa watu mbalimbali kuepuka kunywa dawa za asili zinazotembezwa mitaani kwa kuwa nyingine hazina ubora na zina madhara kwa afya ya binadamu

Post a Comment

0 Comments