RAIS KIKWETE AFUNGA SEMINA KWA MAWAZIRI YA UTEKELEZAJI WA MFUMO MPYA WA UTENDAJI SERIKALINI

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akifunga semina kwa mawaziri na makatibu wakuu  walioketi na kupanga mikakati ya utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa  kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Awamu ya kwanza ya labs ilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete  tarehe 22 Februari, 2013 na kukamilika Aprili, 2013. Maeneo ya awamu ya kwanza ya labs yanahusisha elimu, kilimo, nishati, mapato, maji na miundombinu ya uchukuzi.

 Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa benki ya NBC Bw. Lawrence Mafuru akitoa majumuisho ya uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo katika   semina elekezi  kwa mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.

 Mawaziri wa  Fedha, Kilimo, Uchukuzi, Maji, Nidhati na Madini na Elimu wakiweka saini  waraka wa  kujifunga katika utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo uliokabidhiwa kwa wizara sita  hizo sita baada ya  semina elekezi  kwa mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa  kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Awamu ya kwanza ya labs ilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete tarehe 22 Februari, 2013 na kumalizika mwezi huu wa  Aprili, 2013. Maeneo ya awamu ya kwanza ya labs yanahusisha elimu, kilimo, nishati, mapato, maji na miundombinu ya uchukuzi
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe Ombeni Sefue wakiwa na mawaziri na makatibu wakuu wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia Dkt Idris Jala wakti wa kuujadili  mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo uliokabidhiwa kwa wizara hizo sita katika   semina elekezi  kwa mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa  kwa kutumia uzoefu wa PEMANDU, ambapo utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post