Halmashauri ya jiji la Arusha imekiri kukabiliwa na tatizo sugu la msongamano wa watu na magari kitendo
kinachochangia kuaribu sifa ya jiji hilo sanjari na kuvuruga utaratibu mzima wa
maisha ya watu jijini hapa.
Hatua hiyo
imekuja zikiwa ni siku chache tu baada ya mkuu wa usalama barabarani
mkoani Arusha,Marison Mwakyoma kutamka ya kwamba baadhi ya watu binafsi
kujimilikisha vituo vya kuegeshea magari ya abiria kitendo kinachopelekea
usumbufu kwa baadhi ya madereva na wafanyabiashara jijini Arusha.
Akihojiwa na
gazeti hili kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha,Afwilile Lamsy
alisema kuwa tatizo la msongamano wa magari na watu jijini hapa ni sugu na
kwamba limekuwa kero kwa muda mrefu.
Alisema
kwamba tatizo hilo limechangia kwa kiasi kikubwa kuvuruga utaratibu mzima wa
maisha na sifa la jiji la Arusha kwa kuwa baadhi ya baadhi ya magari yamekuwa
yakishusha abiria sehemu ambayo hayaruhusiwi na kuchangia msongamano.
Lamsy,ambaye
anakaimu nafasi ya Omary Mkombole aliyehamishiwa wilayani Babati kuwa
mkurugenzi wa halmashauri hiyo alisema kuwa kufuatia tatizo hilo uongozi wa
jiji hilo unatarajia kuanzisha safari ndefu za magari ya kubeba abiria jijini
hapa kama njia mojawapo ya kuondokana na tatizo hilo.
“Tunatarajia
kuanzisha route ndefu(safari ndefu) za magari tunataka magari yaisiwe yanashusha abiria kati kati ya mji na
sehemu nyingine hovyo hovyo ili kuondoa msongamano”alisema Lamsy
Hatahivyo,alisisitiza
kuwa lengo la kuanzisha safari ndefu litasaidia kuepuka vitendo vya abiria
kufuata magari sehemu ambazo sio vituo vya magari ya abiria vilivyohalalishwa
na uongozi wa jiji hilo.
Katika siku
za hivi karibuni jijini Arusha kumekuwa na utaratibu wa magari ya abiria
hususani daladala kushusha na kupakia abiria katika maeneo ambayo
hayajaruhusiwa kisheria kitendo ambacho kimepelekea usumbufu mkubwa kwa baadhi ya wafanyabiashara
waliopo katikati ya jiji la Arusha.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia