Kinana
akimkabidhi kadi ya CCM Mwanachama mpya wa CCM tawi la Mawasiliano,
Ulanga, Magdalena Mashinga. Kushoto ni Khatibu na mtk wa CCM Moro
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi ya Chadema kutoka kwa
aliyekuwa mwanachama wa chama hicho, Abeid Mloka aliyetangaza kuhamia
CCM, wakati Kinana alipohutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika kijiji
cha Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Mloka alikuwa
miongoni mwa vijana watano walioamua kuahamia CCM papo hapo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika Kijiji cha Mwaya, Ulanga, Morogoro,
Katibu
wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib, akionyesha kadi za Chadema
ambazo vijana waliokuwa wanachama wa chama hicho waliamua kumkabidhi
papo hapo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mkutano mkubwa
wa hadhara uliofanyika Aprili 15, 2013, kwenye Kijiji cha Mwaya,
Ulanga mkoani Morogoro.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitia saini kitabu wageni alipokagua
uhai wa Chama kwenye tawi la CCM la Ulanga mjini,mkoani Morogoro, Aprili
15, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni Mohammed Seif Khatib.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi Mbuzi kwa Nahodha wa timu ya
Libenenga, Steven Maundu, baada ya timu hiyo kuibuka mshindi kwa
kuibugiza timu ya Nkongo mabao 2-0, katika mechi ya fainali ya Kinana
CUP, kwenye Uwanja wa Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013.
Pamoja na zawadi hiyo, ameipatia timu hiyo zawadi ya sh. 100,000 kiasi
kinacholingana na alichoipa timu iliyofungwa. Kulia ni Nahodha wa timu
ya Nkongo, Abdallah Mazengo.
.Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Katibu wa tawi
la CCM Kiwanjani, Ulanga,mkoani Morogoro, Francis Kanyali aliyekuwa
akisoma taarifa, Kinana alipotemebea tawi hilo kukagua uhai wa Chama,
Katibu
wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib akikagua daftari la
wanachama wa CCM kwenye tawi la Mawasiliano, Ulanga mkoani Morogoro,
alipofika hapo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
.
Mwenyekiti wa CCM shina la Mawasiliano, Ulanga, mkoani Morogoro, Petro
Kabisi akiwatambulisha viongozi wa shina hilo kwa Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana aliyetembelea tawi hilo kukagua uhai wa Chama
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa CCM tawi la Ulanga Mjini mkoani Morogoro, baada ya kukagua
uhai wa Chama kwenye tawi hilo,
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Pancras Mogela aliyekuwa
mwanachama wa Chadema akipoamua kujiunbga na CCM, Kinana alipotembelea
tawi la CCM Viwanjani, Ulanga mkoani Morogoro, kukagua uhai wa Chama
kwenye tawi hilo. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed
Seif Khatib.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kucheza ngoma ilkiyokuwa
ikipigwa na kina mama, kwenye tawi la CCM Nawenge Ulanga, alipowasili
kwenye tawi hilo kukagua uhai wa Chama
Wananchi
wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa
hadhara wa CCM uliofanyika Aprilki 15, 2013 kwenye Uwanja wa Mwaya,
Ulanga mkoani Morogoro.