BREAKING NEWS

Wednesday, April 3, 2013

SEREKALI YACHACHAMAA


Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa  
Tayari imekwishaiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuwachunguza, ili kuona kama hawajavunja sheria.

Kwa mujibu wa tamko la Serikali lililosainiwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, kwa muda mrefu sasa, wamiliki hao wamekuwa wakivitumia vyombo vyao kupotosha umma juu ya mfumo huo wa dijitali.

“Serikali haitavumilia kikundi au mtu yeyote atakayeonekana kuwa anapotosha au kufifisha mchakato wa kuhamia katika mfumo wa utangazaji wa dijitali. Serikali inaiagiza TCRA kuendelea na utaratibu, ratiba ya zoezi zima la uzimaji wa mitambo ya analojia kama ilivyotolewa na Serikali,” lilisema tamko.


Tamko hilo limeitaka TCRA, kupitia Kamati ya Maudhui ku chunguza kama kauli zilizotolewa na baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari katika vyombo vyao, hazikukiuka sheria na kanuni za utangazaji kwa lengo la kupotosha umma ili kudhoofisha uiamuzi ya Serikali.”
Lilisema hivi wamiliki hao wamekuwa wakitoa kwa nguvu, kauli za kupotosha kupitia katika mikutano ya waandishi wa habari na katika mijadala ndani ya baadhi ya redio na televisheni.

“Kauli hizo zimetia hofu vyombo vya fedha ambavyo vimekuwa vikitoa mikopo kwa wajenzi wa miundombinu ya urushaji wa matangazo katika mfumo wa dijitali,” ilisema sehemu ya tamko hilo la Serikali.

Pia lilisisitiza kuwa kauli hizo si za kweli na kwamba zinalenga katika kuchochea wananchi wasikubaliane na uamuzi wa Serikali.
Linasema kuwa, Serikali itaendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kwa kutumia njia mbalimbali, ili kufikia Juni 17 mwaka 2015 , Tanzania iwe imekamilisha uhamiaji katika mfumo dijitali.

Linasema kwamba, wamiliki hao walikuwa na miaka saba ya kuwasilisha maoni au malalamiko yao katika mamlaka zinazohusika ili yaweze kufanyiwa kazi.

Hata hivyo lilisema Serikali iko tayari kushirikiana na wamiliki hao katika kutatua changamoto zinazowakabili ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mpango wa kuhamia katika mfumo wa utangazaji, unaendelea kama ilivyopangwa, badala ya kutumia muda mwingi kupotosha umma.

“Ikumbukwe kuwa mabadiliko haya hayaepukiki, hivyo basi wadau wote kwa pamoja hawana budi kushirikiana katika mchakato mzima kama ilivyokubalika kupitia vikao mbalimbali vilivyofanyika tangu mwaka 2005,” ilisisitiza sehemu ya tamko.
Mwezi uliopita, Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari vya Utangazaji (MoaT), kilitishia kuzima mitambo ya vituo vya televisheni kwa maelezo kuwa wamiliki wake hawawezi kuviendesha kwa hasara.

Mwenyekiti wa chama hicho, Reginald Mengi, alisema vituo hicho sasa vinaendeshwa kwa hasara baada ya watangazaji kusitisha kutangaza biashara zao kufuatia kitendo cha wanchi wengi kushindwa kununua ving’amuzi vya kuwawezesha kuangalia vipindi.

Aliishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kuruhusu vituo hivyo kuendesha shughuli zake kwa kutumia mifumo yote miwili (analojia na dijitali), ili kuwawezesha wananchi wengi, kuangalia televisheni,hatua ambayo itavutia utangazaji wa kibiashara.

Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Mawasilioano,Profesa John Mkoma, alisisitiza kuwa kama Serikali haitarejesha mfumo wa zamani wa matangazo kwa njia ya analojia na kwamba mfumo huo lazima ukome.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates