JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI
TANZANIA
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
KUTOKA OFISI YA
KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
TUKIO
LA AJALI YA MAPOROMOKO YA MORAMU ILIYOSABABISHA VIFO VYA WATU KUMI NA TATU
MNAMO TAREHE
01/04/2013 MUDA WA SAA 4:40 ASUBUHI HUKO MOSHONO TANGANYIKA PARKERS KWENYE
MACHIMBO YA MORAMU, WATU KUMI NA TANO (15) WAKIWA KATIKA UCHIMBAJI NA UPAKIAJI
WA MORAMU WALIANGUKIWA NA KIFUSI CHA UDONGO WA MORAMU NA HATIMAYE KUSABABISHA VIFO VYA WATU KUMI NA
TATU (13) NA WAWILI KUJERUHIWA.
TAARIFA HIZO
ZINAELEZA KWAMBA, MUDA WA SAA 4:00 ASUBUHI WATU HAO WALIKUWA WANAPAKIA MORAMU
KATIKA MAGARI MAWILI AMBAYO NI SCANIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 886 BDA NA JINGINE NI AINA YA MITSUBISHI FUSO LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 109 AYB.
ILIPOFIKA MUDA HUO WA
ASUBUHI, KIFUSI CHA MORAMU KILIPOROMOKA GHAFLA NA KUWAFUNIKA WATU WOTE
WALIOKUWA KATIKA ENEO HILO. MPAKA HIVI
SASA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA LIMETAMBUA MIILI YA MAREHEMU PAMOJA NA
MAJERUHI. WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO NI:- JULIUS S/O PETER PALANGYO (56) MKAZI WA NKOARANGA WILAYANI ARUMERU,
FREDY S/O LOSERIAN (21) MKAZI WA
TANGANYIKA PARKERS MOSHONO, CHRISTOPHER
S/O LAURENT (24) KONDAKTA NA NI MKAZI WA KIJENGE, GERALD S/O JACOB MAARUFU KWA JINA LA KABABU (24) MKAZI WA MOIVARO, GERALD S/O MASAI (33) MKAZI WA
TANGANYIKA PARKERS, JAPHET S/O AMANI
KIVUYO (27) MKAZI WA MOSHONO NA MWENDA
S/O STEPHANO (25) MKAZI WA MOIVARO.
WENGINE NI ELIAS S/O FANUEL (28) MKAZI WA
TANGANYIKA PARKERS, BARICK S/O KIPARA
(26) MKAZI WA MOSHONO, SEURII S/O
RAPHAEL MAARUFU KWA JINA LA MBU (24) MKAZI WA MOSHONO, ALEX S/O MARICK (23) DEREVA NA NI MKAZI WA MOSHONO, HASSAN S/O MUSSA (24) MKAZI WA MOSHONO
NA WA MWISHO NI GERALD S/O NERUJANGI
(45) MKAZI WA MOSHONO.
MAJERUHI KATIKA
AJALI HIYO NI SAMWEL S/O GUNDA (29)
KONDAKTA, MKAZI WA MOSHONO NA MARIAKI
S/O LENANU (48) MKAZI WA TANGANYIKA PARKERS AMBAO WOTE WALIKUWA WAMELAZWA
KATIKA HOSPITALI YA MOUNT MERU HIYO JANA NA SAMWEL S/O GUNDA AMESHARUHUSIWA HUKU MWENZAKE AKIENDELEA KUPATIWA
MATIBABU. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI CHA
HOSPITALI YA MOUNT MERU. ASANTENI KWA
KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA
NA KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI,
(ACP)
IBRAHIM KILONGO
TAREHE
02/04/2013
|
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia