Barabara rasmi kutoka
mji mkuu Mogadishu, kuelekea mji muhimu wa Kusini Magharibi mwa nchi
Baidoa, umedhibitiwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika kutoka kwa
wapiganaji wa kiisilamu.
Ni mara ya kwanza kwa barabara inayounganisha miji hiyo kuwa wazi kwa zaidi ya miaka miwili.
Muungano wa Afrika unasaidia serikali mpya ya Somalia kudhibiti eneo hilo kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu wa Al Shabaab.
Kundi hilo limelazimika kuondoka katika miji mikubwa lakini wangali wanadhibiti vijiji na maeneo mengi ya mashinani.
Sehemu ya mwisho ya barabara hiyo kutoka
Mogadishu, ilidhibitiwa siku ya Jumatatu , kwa mujibu wa muungano wa
Afrika ambao una majeshi 18,000 nchini humo.
Muungano huo ulisema kuwa hatua hii muhimu
hairuhusu tu uhuru wa watu kutembea, lakini pia inafungua njia ya
kusafirishia msaada wa kibinadamu.
Wakati huoho, mlipuko ulitokea mjini Mogadishu,
katika ofisi ya Dahabshiil, moja ya kampuni kubwa za biashara ya kutuma
pesa barani Afrika,
Mtu mmoja alijeruhiwa wakati wa shambulio hilo.
Haijulikani aliyehusika na shambulio hilo lakini
kampuni hiyo ilitishia kufunga ofisi zake katika maeneo yanayodhibitiwa
na al-Shabab.
Licha ya shambulio hilo, hali imeimarika mjini
Mogadishu tangu al-Shabab kuondoka mjini humo mwezi Agosti, , lakini
wapiganaji wake wangali wanafanya mashambulizi ya kuvizia.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia