Ras Makunja na kicheko chake ...!
Wataalamu wa mambo ya afya wanasema kucheka ni afya! sijui kama kweli au lah?
Nchini india kuna vilabu vya kufanya mazoezi ya
kucheka,pia katika nchi nyingi kuna wasanii wachekeshaji
(Comedy)wanaofanya vituko kuwawezesha wanadamu wengine wacheke,inamaana
kucheka ni tiba ya kuondoa fikira mbaya katika nafsi au? na wasanii wetu
wa vichekesho nao ni madaktari.
Lakini tunajiuliza hivi kila anaeonyesha meno
anacheka au? kama kamanda Ras Makunja wetu (pichani) juzi juzi alikua
studio kupika nyimbo akafumwa akicheka sana sana kiasi ya watu
waliokuapo pale walikua wakijiuliza hivi kicheko cha kamanda meno nje!
ni kicheko kweli au ? tukae mkao wa kula kusikia ujio wa vitu vipya kwa
siku za usoni.
lakini acha tuendelee kupata raha