
Halmashauri ya Meru wilaya ya Arumeru imeshika nafasi ya Tano
kitaifa na ya kwanza kimkoa na kuzibwaga halmashauri zote sita za mkoa
wa Arusha katika matokeo ya kidato cha pili yaliyotoka mapema wiki hii.
Akizungumza na mwandishi wetu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya
Meru mwalimu Damari Mchome amesema kuwa Halmashauri ya Meru imeshika
nafasi ya Tano kati ya halmashauri 175 za Tanzania bara na kuifanya
halmashauri hiyo kushika nafasi ya kwanza kimkoa.
Afisa Elimu Mchome ameongeza kuwa kati ya wanafunzi 5,096 waliofanya
mtihani wa kidato cha pili mwa 2017 wanafunzi 1,278 wamepata daraja la
kwanza, 760 daraja la pili, 874 daraja la tatu na 1,902 daraja la nne
kuifanya alama ya ufaulu ya GPA ya 3.185
Akielezea siri ya ufaulu huo Mchome amesema kuwa halmashauri ina
walimu wa kutosha kwenye masom ya sanaa pamoja na sera ya elimu bila
malipo inayosababisha wanafunzi kuhudhuria masomo bila usumbufu wa
kudaiwa "Baada ya serikali kutoa elimu bila malipo wanafunzi wamekuwa
wakihudhuria darasani bila kukosa tofauti na hapo awali walipokuwa
wanakosa masomo kwa kushindwa kulipa ada na michango mingine jambo
lililochangia ufaulu kwa wanafunzi hao" amefafanua Afisa Elimu
Hata hivyo Halmashauri imepokea jumla ya wanafunzi 5,404 wa kidato
cha kwanza mwaka 2018 wavulana 2,540 na wasichana 2,862 kwenye shule 29
za serikali.
Afisa Elimu taaluma Abernego Mlokozi amesema kuwa wanafunzi hao 5,404
wamegawanywa kwenye mikondo 92 na tayari wanafunzi hao wameanza mafunzo
ya awali ikiwemo matumizi ya lugha ya Kiingereza yatakayofanyika kwa
wiki nane kwa lengo la kuwajengea msingi wa lugha hiyo itakayotumika
kufundishia masomo yote kasoro somo la Kiswahili.
Mulokozi ameongeza kuwa halmashauri imepokea vitabu vya kufundishia
mafunzo hayo ya awali kwa uwino wa kitabu kimoja kwa mwanafunzi