DR. MWIGULU AONGOZA OPERESHENI MASHAMBA YA BHANGI YALIYOPO MAFICHONI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba akishuka
kwenye moja ya mteremko mkali kuelekea kwenye mashamba ya bhangi
yaliyopo mafichoni katika kijiji cha Engalaoni kata ya Musa wilayani
Arumeru
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba akiwa pamoja na Kamanda wa Polisi wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu kamishna (DCP) Charles Mkumbo wakati wa operesheni ya kuharibu mashamba ya bhangi iliyofanyika jana kwenye mashamba yaliyopo katika kijiji cha Engalaoni Kata ya Musa wilaya ya Arumeru.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba akiwa pamoja na Kamanda wa Polisi wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu kamishna (DCP) Charles Mkumbo wakati wa operesheni ya kuharibu mashamba ya bhangi iliyofanyika jana kwenye mashamba yaliyopo katika kijiji cha Engalaoni Kata ya Musa wilaya ya Arumeru.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba jana aliongoza operesheni ya kuharibu
mashamba ya bhangi yaliyopo mafichoni iliyofanyika katika kijiji cha Engalaoni
kata ya Musa tarafa ya Muklati wilayani Arumeru.
Akizungumza katika mashamba hayo ambayo
yamelimwa nyuma ya milima ambayo yapo umbali mrefu na makazi ya watu, Dr.
Mwigulu alitoa tahadhari kwa wananchi wanaojihusisha na kilimo hicho huku
akisisitiza serikali itaendelea kupambana nao na kuwafikisha Mahakamani.
“Natoa tahadhari kwa
wananchi wote wanaolima zao hilo ambalo halikubaliki kwamba, vita hii ni vita
endelevu na wamiliki watafikishwa Mahakamani”. Alionya Dr. Mwigulu na kushauri
kwamba wanachi wanatakiwa kubadilika na kulima mazao mbadala ambayo
yanakubalika kama vile Pareto, Viazi mviringo, na Karoti.
Alisema wale wote
ambao wanaendelea kutoa vyombo vyao vya
usafiri kwa ajili ya kusafirisha zao hilo haramu wajue wanatenda kosa na
wakikamatwa vyombo vyao vitataifishwa.
Dr. Mwigulu alimtaka
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha aendelee kusonga mbele na timu yake huku akimpongeza
kutokana na operesheni za mafanikio alizozifanya hasa za matumizi ya silaha na
mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.
Akizungumza katika
Operesheni hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa
Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles
Mkumbo alisema kwamba, zoezi la kutafuta mashamba ya bhangi yaliyopo kwenye
maficho ni endelevu.
Alisema wananchi
wanatakiwa waachane na kilimo cha zao hilo kwani Jeshi la Polisi lina mtandao
mkubwa wa kubaini uhalifu kwani popote watakapolima watagundulika na kuongeza kwamba, wakulima wa zao hilo
wataendelea kuteseka kwa kukimbia kimbia lakini mwisho wa siku watakamatwa na
sheria kuchukua mkondo wake.
Akizungumzia juu ya
tahtmini ya uelekeo wa mafanikio ya Operesheni hizo hasa katika wilaya ya
Arumeru, Kamanda Mkumbo alisema kwa sasa udhibiti umekuwa mkubwa tofauti na
awali ambao unasababisha wahalifu hao kukimbilia mafichoni badala ya mashamba
yaliyo katika maeneo ya wazi na kusisitiza kwamba, Jeshi hilo litaendelea
kubandika mguu pale ambapo wao watakuwa wananza kulima.
Jumla ya hekari
zilizokadiriwa sita ziliharibiwa kwa kufyekwa ambapo vikosi vya Jeshi la Polisi
kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo mkoani hapa pamoja na wilaya ya Arumeru
viliungana na kufanikisha kazi hizo baada ya kupanda milima mirefu kwa muda wa
saa mbili kutoka walipoacha magari.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia