
Idadi ya Mifugo (Ng'ombe)iliyopo kwenye Halmashauri ya Meru
yapungua, hayo yamebainishwa na Mkuu wa Idara ya Mifugo kwenye
Halmashauri hiyo Dkt.Amani Sanga amesema "Makadirio ya idadi ya Ng'ombe
kwa mwaka 2011 yalionesha kuwa kwenye Halmashauri ya Meru kuna idadi
ya ng’ombe wa asili 151,878, ng'ombe wa maziwa 83,346 jumla 235,224
tofauti na uhalisia tunao ubaini kwenye zoezi hili la upigaji chapa
mifugo idadi hiyo kupungua kutokana na uhaba wa maeneo ya malisho
nakusababisha wafugaji wengi kuhamishia mifugo yao kwenye wilaya zenye
maeneo ya malisho pia baadhi ya wafugaji wamebadili shughuli za
Kiuchumi kwa kua wakulima na wafanyabiashara"
Dkt.Sanga ameeleza kua idara yake imejipanga kuhakikisha zoezi la upigaji chapa Ng'ombe litakamilika kabla
ya tarehe 01 Februari 2017 kwa kujigawa kama timu na kutoa hamasa kwa
wafugaji wote kushiriki zoezi hili kutokana na taratibu zilizopangwa
kwenye kila kijiji.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Christopher J. Kazeri
amewataka wataalamu wanao fanya kazi ya upigaji chapa Mifugo
kuhakikisha Ng'ombe wote waliopo kwenye Halmashauri hiyo wanapigwa chapa
kabla ya Muda wa ukomo .
Aidha zoezi hilo ya upigaji chapa linaloendelea kwenye Halmashauri ya
Meru na kwa leo limefanyika katika Kata ya Ngabobo ambapo jumla ya
Ngombe 1881 wamepigwa chapa hivyo kupeleke idadi ya Ng'ombe wote walio
pigwa chapa kwenye Halmashauri hiyo kufikia elfu 14,055
Picha za tukio hilo

Mkuu wa idara ya Mifugo Dkt. Amani Sanga wakati wa zoezi la upigaji chapa kwenyekijiji cha Oltepesi kilichopo Kata ya Ngabobo.

Afisa mifugo wa Kata ya Ngabobo Ramadhani Maadili akichukua takwimu
toka kwa wafugaji wa kijiji cha Oltepesi Kata ya Ngabobo wakati wa zoezi
la upigaji chapa..

Afisa Mifugo Asanterabi Urasa akipiga chapa ng'ombe wa kijiji cha Oltepesi Kata ya Ngarenanyuki

Dkt.Charles Msigwa akipiga chapa ng'ombe wa kijiji cha Oltepesi Kata ya Ngarenanyuki


Kundi mojawapo ya makundi mengi ya Ngombe likielekezwa eneo la kupigia chapa