CCM MUFINDI WASHEREKEA MIAKA 41 KWA KUTOA MSAADA KWENYE VITUO VYA WATOTO YATIMA

 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Daudi Yassin akiwa na viongozi wa chama hicho wakikabidhi msaada waliupeleka wakati wa kutimiza miaka 41 ya chama cha mapinduzi
 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Daudi Yassin akiwa na viongozi wa chama hicho wakikabidhi msaada waliupeleka wakati wa kutimiza miaka 41 ya chama cha mapinduzi huku wakiwa wameonyesha moja ya msada walioupeleka kwa watoto yatima na hayo ni maziwa yanayozalishwa na kampuni ya Asas
  Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Daudi Yassin akiwa na viongozi wa chama hicho wakikabidhi msaada waliupeleka wakati wa kutimiza miaka 41 ya chama cha mapinduzi huku wakiwa wameonyesha moja ya msada walioupeleka kwa watoto yatima na hayo ni maziwa yanayozalishwa na kampuni ya Asas
 Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi wakiwa wamebeba misaada waliyokuwa wanaipeleka kwenye vituo vya watoto yatima
 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Daudi Yassin akiwa na viongozi wa chama hicho wakikabidhi msaada waliupeleka wakati wa kutimiza miaka 41 ya chama cha mapinduzi
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Daudi Yassin akiwa na viongozi wa chama hicho wakikabidhi msaada waliupeleka wakati wa kutimiza miaka 41 ya chama cha mapinduzi wakiwa na mmoja ya viongozi wa kituo cha watoto yatima wa kituoa cha Makalala

NA FREDY MGUNDA,MUFINDI.

CHAMA cha mapinduzi wilaya ya Mufindi kimesherekea miaka 41 ya chama hicho kwa kufanya kazi za kijamii kwa kwenda kuwatembea watoto yatima wa vituo viwili vilivyopo katika halmashauri ya Mji wa Mafinda kwa kusikiliza kero zao na kutoa msaada wa vitu mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada kwenye kituo cha makao ya watoto Lutheran kinachomilikiwa na kanisa la KKT na kituo cha makao ya watoto Makalala kinachomikiwa na kanisa la kikatoriki ambavyo vyote  vipo katika halmasahuri ya Mji wa Mafinga,mwenyekiti wa chama hicho, Daudi Yasini alisema kuwa chama cha mapinduzi kinasherekea miaka 41 kwa kufanya kazi za kijamii kama alivyoagiza mwenyekiti wa chama hicho taifa.

“Mwaka huu imekuwa tofauti na miaka ya nyuma safari hii ni kufanya kazi kwa kuwatumikia wananchi hivyo tunapaswa kufanya kazi kwa vitendo hivyo naombeni wananchi na viongozi kufanya kazi kwa kujituma na kuhakikisha tunatimiza malengo ya ilani yetu” alisema Yassin

Yassin alisema kuwa wameamua kutembelea vituo vya watoto yatima kwa lengo la kuitaka jamii kwa ujumla kuwa kumbuka watoto hao ambao wanamahitaji mengi huku wakikumbana na changamoto nyingi za kimaisha katika vituo wanavyoishi.

“Mmejione wenyewe kuwa hawa watoto wanaishi kwa kutegemea misaada hivyo tunapaswa kuijenga jamii kwa kujitolea misaada mbalimbali kwa kuwasaidia watoto yatima na wale wanaishi katika mazingira magumu” alisema Yassin

Aidha Yassin alisema kuwa chama cha mapinduzi kinachukizwa na vitendo vya kikatili kwa watoto akina mama hata akina baba hivyo ni lazima jamii ikomeshe vitendo vyote vya ukali wa kijinsia ili kuwa na jamii inatazama maendeleo.

“Jamani hakuna kitu ambacho chama chetu hatupendi kama kusikia maswala ya ukatili wa kijinsia tunaomba jamii ibadilike mara moja na kuwa jamii inayoogopa na kupinga ukatili wa kijinsia,niwaombe watanzania kwa ujumla tukatea ukatili wa kijinsia” alisema Yassin

Kwa upende wake katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Elirehema Nassar alisema kuwa wametoa msaada unaogharimu zaidi ya shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwajali wananchi na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

“Sisi lengo letu ni kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazuri na kukifurahili chama chetu,tumeleta hii misaada ambayo inatasaidia kwa kiasi furani kuwapa faraja watoto na viongozi wa vituo hivi ambavyo tumevitembelea hii leo” alisema Nassar

Nassar alisema kuwa chama hicho haitawavumia viongozi na watu ambao watakwamisha juhudi za Rais John Pombe Magufuli za kuwaletea maendeleo watanzania.

“Nitapambana nao kwa kasi zangu zote na nguvu zote kwa wale ambao watakuwa wanaleta mambo ya ajabu katika jamii kwa kujifanya yeye anajua kuliko viongozi wa serikalia au anapinga kila kitu kinachofanywa na Rais wetu” alisema Nassar
Philipo Kamoga na Helena Msefe Walikipongeza chama cha mapinduzi kwa kutimiza miaka 41 kwa kufanya kazi za kijamii ambazo zinasaidia kutatua changamoto ambazo zinawakabili wananchi wa kipato cha chini.

“Kwanza tunaopenga kwa dhati kwauwa chama cha kwa hapa nchi kufikisha miaka 41 ambayo haijafikiwa na chama chochote kile hapa nchini hongereni sana” walisema viongozi hao


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post