MRADI WA KOICA KUWAWEZESHA MABINTI WAFANYA MKUTANO

WADAU wa mradi wa kuwawezesha mabinti na wanawake vijana katika sekta ya elimu wamekutana katikati ya wiki kujadili mpango kazi wa utekelezaji wa mradi wa UNESCO kwa kushirikiana na UNWomen pamoja na UNFPA unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Korea (KOICA). Mradi huo ambao umelenga kuondoa vikwazo vya elimu kwa wasichana na wanawake kwa kuangalia sera, sheria na kanuni zinazowezesha maendeleo kwa wanawake kwa kuzingatia matakwa ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya kimataifa ambayo Tanzania imetia saini ulianza mwaka 2016. Mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kwa kusimamiwa na Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN Women) na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya Watu ( UNFPA) unatarajia kuiwezesha Tanzania kuwezesha elimu kwa kutumia mbinu mtambuka kwa kutambua watu wa pembezoni. Kaimu Mkuu wa ofisi na Mkuu wa kitengo cha Elimu ofisi ya Unesco Dar es Salaam, Faith Shayo akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ukimwi ofisi za Unesco Dar es Salaam, Mathias Herman.[/caption] Mradi huo unatarajiwa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kuwa na uwezo wa kuingia katika utuuzima bila kuvurugwa utaratibu wa upatikanaji wa elimu. Mradi huo unatekelezwa katika wilaya nne za Ngorongoro, Sengerema, Kasulu na Mkoani huko Pemba. Mkutano huo wa kamati ya ufundi ya mradi ulilenga kutoa ratiba ya utekelezaji wa mradi baada ya mada mbalimbali kuwasilishwa za utafiti uliofanyika na hali halisi iliyopo nchini kuhusu wasichana na wanawake kwa kuangalia sharia zilizopo, utamaduni na tabia. Akizungumza katika mkutano huo Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) Kitivo cha Elimu, Dk. Felix Mulengeki alisema kwamba mradi huo utafanikiwa kutokana na ukweli kuwa sharia na katiba za nchi zipo vizuri huku sera nazo zikitambua haki ya kusoma. Ofisa wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ukimwi ofisi za Unesco Dar es Salaam, Mathias Herman akiwasilisha taarifa ya mwaka 2017 ya mradi huo wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.[/caption] Wakati mradi unabuniwa ilionekana kwamba kutoeleweka kwa katiba na sheria zilizopo zinazomlinda mtoto wa kike, uelewa hafifu umekuwa ukikwamisha maendeleo kielimu kwa watoto wa kike. Dk. Mulengeki alisema kwamba hali ya sera na sheria nchini Tanzania ni salama zaidi kilichobaki utekelezaji wa mradi huo umelenga kukusanya pia takwimu kwa ajili ya kutumika kutengeneza sera. Katika mradi huo unatarajiwa kuongeza uelewa zaidi wa elimu ya afya ya uzazi na kutengeneza mifumo ya kuelimisha watu. Mada mbalimbali zilizojadiliwa ziliwezeshwa kupata muda wa utekelezaji wa vipengele mbalimbali ambavyo vilipaswa kufanyika ili kuondokana na tabia mbaya ambazo zinamnyima binti wa Kitanzania kukamilisha elimu yake.] Washiriki wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu wakifuatilia ripoti ya mwaka 2017 ya mradi huo iliyokuwa ikiwasilisha Mathias Herman kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.[/caption] Naye Kaimu Mkuu wa ofisi na Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) ofisi za Dar es Salaam, Faith Shayo amesema kwamba mkutano huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo na kwamba kamati ya ufundi ya mradi huo ilikutana mara ya kwanza Mei mwaka jana. Naye Ofisa wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ukimwi ofisi za Unesco Dar es Salaam, Mathias Herman anasema kwamba kuna matokeo chanya ya mradi huo. Anasema kwamba madhila mengi ya mabinti katika wilaya hizo zinazofanyiwa utekelezaji wa mradi yamepungua na hali zao kuwa bora kutokana na taasisi mbalimbali zinazohusika na elimu na usalama wa watoto wakike kushirikiana kukabili matatizo waliyonayo. Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) Kitivo cha Elimu, Dk. Felix Mulengeki akiwasilisha mada kuhusu sheria na taratibu zinazogusa elimu ya watoto wa kike wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.[/caption] Pia amesema katika suala la elimu ya afya ya uzazi na Ukimwi kumekuwa na mabadiliko kwani taarifa zinakwenda kwa wakati na zinafanyiwa kazi inavyotakiwa na sekta mbalimbali zikiwemo taasisi za kiserikali katika kumsaidia mtoto wa kike Aidha amesema kwamba vitini vya kufundishia elimu mbalimbali ambazo zimo katika mradi zimeshafanyiwa kazi na kusambazwa. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Socologia na Anthropologia, Dk. Nandera Mhando akiwasilisha uchambuzi wa mradi wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO Ofisi za Tanzania, Christophe Legay (wa kwanza kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam Mwakilishi kutoka UN Women, Bi. Usu Mallya akifafanua jambo katika majadiliano wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Mratibu wa Elimu Shule za Msingi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Salvatory Alute (katikati) akishiriki majadiliano wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Ngorongoro, Teresia Irafay akitoa maoni wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Adam Chacha kutoka kitengo cha Elimu ofisi za Unesco Dar es Salaam akiuliza swali wakati wa mawasilisho ya mada mbalimbali katika mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam Picha juu na chini ni washiriki wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post