Watford ilifunga mabao matatu ya
dakika za lala salama kushinda mechi ya kwanza ya mkufunzi Javi Gracia
dhidi ya Chelsea ,ushindi unaompatia shinikizo kali mwenzake wa Chelsea
Antonio Conte.
Chelsea ilicheza takriban saa moja ikiwa na
wachezaji 10 baada ya Tiemoue Bakayoko kupewa kadi nyekundu baada ya
kucheza visivyo hatua ilioipatia Watford fursa ya kufunga mabao manne.
The
Hornets ambao walikuwa wamepata ushindi mmoja kati ya mechi 12
walizocheza waliongoza kwa utata baada ya Gerard Deulofue kujiangusha
kwa urahisi kufuatia kabiliano la kipa Thibaut Courtois huku Troy
Deeney akifunga mkwaju wa penalti.
Chelsea iliomuingiza Olivier Giroud kwa mechi yake ya kwanza
katika kipindi cha pili ilisawazisha wakati nyota wao Eden Hazard
alipofunga bao zuri akiwa miguu 25 kutoka kwa lango.
Lakini dakika
mbili baadaye ,Daryl Janmaat alifunga bao zuri wakati alipochenga
kutoka wingi ya kulia na kucheza moja mbili na Robert Pereyra
akawachenga mabeki wengine kabla ya kufunga na mguu wake wa kushoto.
Deulofeu
aliongeza bao lake la pili wakati alipotamba na mpira na kushambulia
kabla ya mpira kumpiga beki Gary Cahill na kuingia.
Watford sasa
wako pointi sita juu ya eneo la kushushwa daraja.Gracia ambaye alichukua
mahala pake marco Silva mwezi uliopita aliambia bbc Sport: Ulikuwa
ushindi mkubwa na mechi nzuri, Nawapongeza wachezaji wangu.Tulicheza
mechi nzuri , tukawasukuma sana.
''Mechi ilibailika baada ya kadi
nyekundu kutolewa lakini nadhani tulicheza vyema. Chel;sea ni klabu
kubwa sana , na timu kubwa''.